Na Afisa habari- Mwanza.
Serikali
mkoani Mwanza imelaa ni mauwaji yaliyofanywa na mfanyabiashara maarufu
jijini humo Jumanne Mahende(J4) hivi karibuni katika eneo la Nyakato
Sokoni katika Wilaya ya Ilemela mkoani humo.
Tamko
hilo limetolewa na mkuu wa mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo wakati
akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake mapema hivi leo, akitoa
tamko hilo mbele ya waandishi wa habari, Mkuu wa mkoa wa Mwanza amesema
sio kitendo kinacho kubalika wala kuhalalishwa na mtu yeyote mwenye
roho ya binadamu.
Mulongo
amesema, hata wavumilia wala kuwachekea watu wanao thubutu kutoa uhai
wa mtu kwa kisingizio cha madeni, “nataka wananchi wafahamu hakuna
mbadala wa uhai wa mtu, kama Serikali ya mkoa, wataiomba mahakama iweze
kutenda haki pale ambapo ushahidi utakapojitosheleza ili haki
ipatikane.
Aidha,
amesema hakuna mtu aliye juu ya sheria na kuamua kutoa uhai wa mtu
mwingine. ”Ndugu zangu nataka kila mmoja wetu afahamu hakuna mbadala wa
maisha au uhai wa mtu, haiwezekani mtu afanye mauwaji halafu aachwe
aendelee kutamba kwa kusema yupo karibu na vyombo vya usalama, mimi kama
mkuu wa mkoa nataka umma ufahamu kuwa tunataka kuongoza watu kwa amani
na utulivu na ikitokea mmoja hataki kufuata utaratibu lazima sheria
ifuate mkondo wake.
Alisema
“ kuondoa haki ya mtu kuishi na kufanya wategemezi wa familia kuwa
wategemezi kwa watu wengine kitu ambacho kina dumaza uchumi wa mtu mmoja
mmoja, jamii lakini uchumi wa mkoa na nchi kwa ujumla.
Wakati
huohuo ameiomba jamii ya wanamwanza kutoa ushirikiano wa dhati kwa
kutoa taarifa kwa vyombo vya dola pindi wanapo ona kuna viashiria vya
uvunjifu wa amani huku akiahidi kusimama kidete na kuona haki inatendeka
kikamilifu.
Mbali ya kutoa karipio hilo, mkuu huyo wa mkoa ametumia wasaa huo kutoa taarifa ya uandikishaji wapigakura kwenye daftari la kudumu la wapiga kura kwa mfumo wa BVR katika mkoa huo na kusema mkoa umevuka lengo kwa kufikisha asilimia 103, ambayo ni mafanikio makubwa kutokana na malengo waliyo jiwekea hapo awali.
Alisema hapo awali mkoa ulijiwekea malengo ya kuandikisha watu 1,403,743 lakini kutokana na maandalizi na mipango mizuri ya mkoa wamefanikiwa kuandikisha watu 1,442,391 sawa na asilimia 103.
Akitoa mchanganuo huo kwa kila jimbo alisema Jimbo la Nyamagana wameandikisha watu (273,636). Ilemela (234,879), na Sengerema (153,054), majimbo mengine ni Buchosa (158,510), Misungwi (149,535), Magu (147,155),Kwimba (86,273), Sumve (76,466) na Ukerewe (162,883).
Mkoa wa Mwanza kwa mujibu wa Sensa ya watu wa makaazi ya Mwaka 2012 ulikuwa na watu wapatao Mil.2.7.
0 comments:
Post a Comment