RC DAR AONGOZA HARAMBEE YA WAANDISHI YA MEDIA CAR WASH FOR CANCER DAR ES SALAAM

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Mecky Sadick akiosha pikipiki ya Blogger Mroki Mroki 'Father Kidevu' (kushoto kwake)  wakati wa harambee  kuosha Magari katika viwanja vya Leaders Club kwa ajili ya kuchangia Fedha kwa waandishi wa Habari ambao wanamatatizo ya Kiafya ikiwemo Saratani.
 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda akiosha pikipiki hiyo baada ya kuzidi dau na kufanya jumla ya shilingi 150,000/= kupatikana kwa kuosha pikipiki hiyo.
Mdauhuyu nae alikuja na Baiskeli yake kwaajili ya kushiriki zoezi hilo na baikeli hiyo ilichangiwa 40,000/= ili ioshwe. Daudi Mambya akiosha baiskeli hiyo na kuchangia waandishi.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mh. Meck Sadick akizindua zoezi la kuosha Magari katika viwanja vya Leaders Club kwa ajili ya kuchangia Fedha kwa waandishi wa Habari ambao wanamatatizo ya Kiafya ikiwemo Saratani .
 Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Assah Mwambene akikabidhi kiasi cha fedha kwa Mmoja wa Waratibu wa MEDIA CAR WASH FOR CANCER Bwa.Benjamin Kasenyenda,zilizochangwa na Idara hiyo kupitia chama chao cha Maofisa Habari wa Serikali ,walijitolea kuchanga kiasi cha shilingi Milioni 1,680,000=.Pichani kati anaeshuhudia ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda

Kama vile haitoshi nayo Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na michezo pia walifanikisha kuchangia kiasi cha shilingi 1,350,000/= kufuatia kuguswa kwa namna moja nyingine kwa kampeni  hiyo adhimu ya kuwachangia waandishi wa Habari wenye Matatizo mbalimbali yakiwemo na ya Saratani.

Mbali ya fedha hizo kupatikana pia walijitokeza watu mbalimbali kuunga mkono kampeni hiyo ya MEDIA CAR WASH FOR CANCER,ambalo kwa kiasi kikubwa bado linahitaji kuongeza hamasa zaidi ili wadau wazidi kujitokeza na kuchangia.

Kampeni hiyo imefanyika leo katika viwanja vya Lidaz Club,Kinondoni jijini Dar,ambapo viongozi mbalimbali wakiwemo na wadau wa habari walishiriki zoezi la kuosha magari kwa kuchangia kiasi chochote cha fedha,huku mgeni rasmi akiwa Mkuu wa Mkoa Dar Es Salaam Mh Meck  Sadick. 

Aidha Miongoni mwa taasisi zilizochangia harambee hiyo ni Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Benki ya Posta Tanzania (TPB), Redio 5 ya Arusha, TANAPA, NSSF, NHIF, na wengine wengi pamoja na baadhi ya wabunge, Wakuu wa Wilaya na watu binafsi. 
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh. Paul Makonda akiendelea Kuosha moja ya Magari yaliyofika kuoshwa katika Media Car Wash for Cancer. Ikiwa ni kuchangia waandishi wa habari wenye magonjwa mbalimbali ikiwemo Saratani.
 Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo Zitto Kabwe akiosha Gari Sitti Mtemvu wakati  wa  Shughuli hiyo maalum kwa ajili ya Kuchangia waandishi wenye udhoofu wa afya zao.
Ankali Issa Michuzi wa Libeneke la Michuzi Blog na Michuzi Media Group na Mwana TBN  akiwa Bizeee... Anaosha Moja ya Magari kwa ajili ya kuchangie waandishi wa habari ambao wanamaradhi ya Saratani
Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO,Assah Mwambene akizungumza jambo na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh.Paul Makonda mara baada ya kushiriki zoezi zima la kuwachangia waandishi wa Habari wenye Matatizo mbalimbali yakiwemo na ya Saratani (MEDIA CAR WASH FOR CANCER).


Picha ya pamoja ya waandishi wa Habari pamoja na Baadhi ya Viongozi.
SHARE
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment