Balozi
wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Flaviana Matata, akikabidhi begi kwa mwanafunzi
wa Shule ya Msingi, Nyerere iliyoko Manispaa ya Singida, Oktoba 7, 2015. PSPF
kupitia Sera yake ya kusaidia jamii imetoa msaada wa mabegi na madaftari kwa
shule hiyo na ile ya Chididimo iliyoko nje kidogo ya Manispaa ya Dodoma
NA
K-VIS MEDIA, DODOMA NA SINGIDA.
BALOZI
wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Flaviana Matata, ametoa wito kwa wanafunzi wa
shule za msingi Chididimo iliyoko Manispaa ya mji wa Dodoma na ile ya Nyerere
iliyoko mkoani Singida kuwahimiza wazazi wao kujiunga na Mfuko huo.
Balozi
huyo ambaye pia ni Mwanamitindo wa Kimataifa anayefanyia kazi zake nchini
Marekani, ameyasema hayo kwa nyakati tofauti, wakati akikabidhi vifaa vya shule
kwa wanafunzi hao Oktoba 7, 2015.
“Mimi
kama Balozi wa PSPF, ninatoa wito kwa wanafunzi mliopo hapa, kufikisha ujumbe
huu kwa wazazi wenu, kwani kujiunga na PSPF kuna faida nyingi katika maisha ya
sasa na ya baadae.” Alisema
Alisema,
PSPF inatoa mikopo mbalimbali kwa wanachama wake kama vile ya viwanja, mkopo wa
elimu, na mkopo wa kuanzisha maisha.
Lakini
pia PSPF inatoa mafao mbalimbali kwa wanachama wa Mpango wa Uchangiaji wa
Hiari, yaani (PSS), ikiwemo, Fao la Uzazi, Fao la Uzeeni, Fao la Elimu, Fao la
Ulemavu na Fao la Ujasiriamali.
“Wazazi
wenu wawe wakulima, wafanyakazi walioajiriwa au kujiajiri wanaweza kujiunga na
PSPF kupitia mpango wa Uchangiaji wa Hiari.” Alifafanua Balozi huyo.
Naye
Afisa Masoko Mwandamizi wa PSPF, Rahma Jemina Ngassa, alisema moja ya Sera za
Mfuko huo ni kuchangia sekta ya Elimu na msaada huo ni utekelezaji wa Sera wa
kusaidia jamii.
“PSPF
inaamini vifaa hivyo vitapunguza kwa kiasi Fulani changamoto zilizokuwa
zinawakabili wanafunzi hao na hivyo watakuwa kwenye nafasi nzuri ya ushiriki wa
masomo kikamilifu.” Alisema.
Kwa
upande wake, Kaimu Afisa Elimu Manispaa ya Dodoma, Christopher Ligonda,
ameupongeza Mfuko huo kwa kuwajali wanafunzi ambao wazazi wao kwa namna moja au
nyingine ni wanachama au wanachama watarajiwa na hata wanafunzi wenyewe.
Naye
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Nyerere iliyoko mkoani Singida, Yesaya
Ramadhani, ameushukuru uongozi wa PSPF kwa kuwafikiria wanafunzi wa shule hiyo
katika kuwasaidia vifaa hivyo ambavyo ni mabegi na madaftari kuwa ni kitendo
cha kweli katika kusaidia jamii ambayo inakabiliwa na changamoto mbalimbali.
0 comments:
Post a Comment