Mkuu wa Kitengo cha Elimu kwa Umma, Makao Makuu ya Trafiki, Dar es
Salaam, ASP Abel Swai akitoa elimu ya usalama barabarani kwa abiria,
muda mfupi kabla ya kuanza safari za mikoani katika kituo Kikuu cha
mabasi Ubungo, jijini Dar es Salaam, elimu ambayo inalenga kudhibiti
ajali za barabarani kuelekea kipindi cha mwisho wa mwaka.
Askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani, PC Asha Adam, akiwasisitiza
abiria kufunga mikanda iliyopo kwenye viti walivyoketi muda wote wa
safari muda mfupi kabla ya magari kuondoka katika kituo Kikuu cha
mabasi ya abiria Ubungo, jijini Dar es Salaam, kama hatua ya kudhibiti
majeraha na vifo vitokanavyo na ajali za barabarani, kuelekea kipindi
cha mwisho wa mwaka.
Askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Inspekta Ibrahim Omary
Samwi(kushoto), na PC Elisante Bura(kulia), wakikagua moja ya magari
yanayofanya safari zake mikoani, kutekeleza mkakati wa Jeshi la Polisi
kupitia Kitengo cha Usalama Barabarani kudhibiti ajali kuelekea kipindi
cha mwisho wa mwaka. Zoezi hili limefanyika muda mfupi kabla ya magari
kuondoka katika kituo Kikuu cha mabasi Ubungo,jijini Dar es Salaam
kuelekea mikoa mbalimbali ya Tanzania.
Askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Inspekta Ibrahim Omary
Swami(aliyeko chini ya uvungu wa gari), akikagua moja ya magari
yanayojiandaa kuelekea mikoani, zoezi ambalo limefanyika muda mfupi
kabla ya magari kuanza kuondoka katika kituo Kikuu cha Mabasi, Ubungo
jijini Dar es Salaam.aliyenyoosha kidole juu ni PC Elisante Bura. Hatua
hii ya Jeshi la Polisi nchini linalenga kudhibiti ajali kuelekea
kipindi cha mwisho wa mwaka.
Askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Sajenti Jackson Mafuru (kulia),
na PC Elisante Bura(kushoto), wakikagua moja ya magari yanayofanya
safari zake mikoani. zoezi hili ambalo limefanyika muda mfupi kabla ya
magari kuondoka katika kituo Kikuu cha mabasi Ubungo,jijini Dar es
Salaam, ni moja ya hatua ya Jeshi la Polisi kupitia Kitengo cha Usalama
Barabarani kudhibiti ajali kuelekea kipindi cha mwisho wa mwaka.
Askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Koplo Abdallah Bwasi akikagua moja ya magari yanayofanya safari zake nje ya mkoa wa Dar es Salaam, muda mfupi kabla ya magari kuondoka katika kituo Kikuu cha mabasi Ubungo,jijini Dar es Salaam.Hatua hii ya Jeshi la Polisi kupitia Kitengo cha Usalama Barabarani imekuja kwa lengo la kudhibiti ajali kuelekea kipindi cha mwisho wa mwaka.
(Picha zote na Abubakari Akida, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
Imeandaliwa na Kitengo Cha Mawasiliano ya Serikali- Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
0 comments:
Post a Comment