Uongozi wa Chuo cha Ufundi Arusha (ATC) unautaarifu umma wa Watanzania na Wadau
mbalimbali wa Chuo kuwa, hivi karibuni kumekuwepo na taarifa za tuhuma mbalimbali kwenye
mitandao ya kijamii dhidi ya Menejimenti ya Chuo, Mkuu wa Chuo, Baadhi ya Watumishi na
Mamlaka za Serikali.
Aidha, Uongozi wa Chuo unapenda kukanusha na kueleza Umma kuwa, taarifa hizo hazina
chembe zozote za ukweli na zinazushwa na baadhi ya Watu wachache kwa lengo la kupotosha
Umma na kwa nia ya kudhoofisha ustawi mzuri wa Chuo.
Vile vile tuhuma hizo zimeeleza kuwepo uonevu kwa baadhi ya Watumishi wa Chuo. Tunapenda
Umma ufahamu kuwa, Chuo hakijawahi kumwonea Mtumishi yeyote na maswala yote
yanayohusu watumishi hushughulikiwa kwa mujibu wa sheria na kanuni za Utumishi wa Umma
na nchi ikiwa ni pamoja na wafanyakazi watatu (03) waliofukuzwa kazi kwa kukiuka sheria hizo
na shauri lao liko kwenye Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA).
Mwisho tunapenda kuufahamisha Umma kuwa, wakati wowote Chuo kipo tayari kutoa taarifa
sahihi kwa Mamlaka zilizoko kisheria.
Ofisi ya Uhusiano Chuo cha Ufundi Arusha (ATC)
Barua pepe: pro@atc.ac.tz, tovuti: www.atc.ac.tz
Imetolewa na:
S.L.P 296, Arusha.
0 comments:
Post a Comment