Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu ya Green Bird Education Institute Habibu Foundation, Juma Mndeme (mwenye miwani) akizungumza jambo baada
ya kumaliza kukabidhi misaada ya mabenchi ya kukalia, sabuni na vinywaji kwa
Kituo cha afya Mwanga, wilayani Mwanga mkoani Kilimanjaro. Aliyeshika majaketi
ni Mganga Mkuu Msaidizi wa Kituo hicho Honest Temba na aliyeshika simu ni
Meneja Uhusiano wa Habibu Foundation, Julysiza Mangiseni.
Na Mwandishi Wetu, Mwanga.
MAADHIMISHO ya Siku Maalum ya Habibu Day wilayani
Mwanga, mkoani Kilimanjaro yamefanyika kwa mafanikio kwa kushirikisha matukio
mbalimbali yakiwamo ya kutoa misaada katika kituo cha Afya Mwanga, kutoa
misaada kwa Jeshi la Polisi, pamoja na kufanyika mijadala mbalimbali ya kielimu
iliyoendeshwa na wanafunzi wa shule za sekondari wilayani humo.
Katika mijadala, wanafunzi hao walitumia muda mwingi kuzungumzia mfumo wa kielimu
nchini Tanzania sanjari na upangaji wa matokeo ya mitihani kutoka Division na
GPA iliyoondolewa rasmi katika mfumo huo nchini hapa, huku mgeni rasmi akiwa ni
Mkurugenzi wa Chuo Kikuu cha Jomo Kenyata kilichopo Arusha, Profesa Ward
Mavura.
Meneja Uhusiano wa Taasisi ya Elimu ya Green Bird Education Institute & Habibu Foundation, Julysiza Mangiseni, akizungumza jambo kwenye maadhimisho hayo yaliyoanzia kutoa zawadi mbalimbali.
Mkurugenzi Mkuu wa Habibu Foundation akizungumza
Mkuu wa Polisi wilayani Mwanga, Pili Mande akipokea sehemu ya zawadi kutoka kwenye Taasisi ya Elimu ya Green Bird
Baadhi ya
wanafunzi wa Chuo cha Green Bird kilichopo wilayani Mwanga wakielekea kwenye
Kituo cha Afya cha Mwanga kwa ajili ya kupeleka zawadi mbalimbali kama ishar ya
kumuenzi muasisi wao marehemu mzee Habibu Mndeme.
Awali ratiba ilianza rasmi saa 12 asubuhi kwa wanafunzi wa shule za
sekondari za Green Bird Girls, Green Bird Boys, Green Bird Collage
zinazomilikiwa na taasisi ya Habibu Foundation kutembelea katika maeneo ya
Ofisi ya polisi Mwanga na kituo cha afya Mwanga, pamoja na kutoa misaada kama
vile mabechi ya kukalia wagonjwa, sabuni, vinywaji pamoja na vifaa ya ofisi kwa
jeshi la Polisi Mwanga.
Akizungumza
katika maadhimisho hayo, Mkurugenzi Mkuu wa wa Taasisi ya Elimu ya Green Bird
Education Institute & Habibu Foundation,, Juma Habibu Mndeme, alisema
kwamba lengo la kufanyika kwa maadhimisho hayo ni kukutanisha pamoja wadau wa
elimu wilayani Mwanga sanjari na kumuenzi mwanzilishi wa taasisi yao marehemu
Habibu Mndeme aliyefariki Dunia mwaka 2010) na kuacha taasisi hiyo inayomiliki
pia shule wilayani Mwanga.
“Tumekuwa
tukiadhimisha matukio haya kila mwaka lakini tunaendelea kuboresha hatua kwa
hatua, maana lengo la taasisi ni kukuza kiwango cha elimu kwa wilaya ya Mwanga
na Tanzania kwa ujumla, ndio maana mijadala ya kielimu ilihusisha wanafunzi
mbalimbali kutoka ndani ya Mwanga na nje pia, ikiwamo jijini Arusha.
“Sisi kama
waendeshaji wa shule zote za Green Bird tunajivunia kufanyika maadhimisho haya
kwa mafanikio makubwa, bila kusahau ulinzi madhubuti kutoka kwenye jeshi la
polisi kuanzia asubuhi hadi usiku, huku tukiona ushindani mkubwa, uzoefu na
umakini kwa kila aliyeshiriki kuonyesha ujuzi na uwezo wake, hususan katika
suala zima la kielimu,” Alisema Mndeme.
Naye Mgeni
rasmi wa maadhimisho hayo Profesa Ward Mavura ambaye pia ni Mkurugenzi wa Chuo
Kikuu cha Jomokenyata cha jijini Arusha, aliitaka jamii ya wilaya Mwanga
kuiunga mkono taasisi hiyo kwa ajili ya kuiweka katika mazingira mazuri katika
utoaji wa huduma zake.
Akizungumzia
tukio hilo na utoaji misaada kwenye jeshi la Polisi wilayani Mwanga, Mkuu wa
Polisi Mwanga, Pili Mande, aliishukuru Taasisi ya Habibu kwa kuwekeza katika
elimu na kuisaidia jamii kwa mambo mengi, jambo linalotakiwa kuungwa mkono na
kuendelezwa kwa manufaa ya Mwanga na Tanzania kwa ujumla.
Naye Meneja
Uhusiano wa wa Taasisi ya Elimu ya Green Bird Education Institute & Habibu
Foundation,, Julysiza Mengiseni, alisema kwamba kufanyika kwa mafanikio kwa
maadhimisho hayo ni hatua nzuri ya kuhakikisha dira ya kuifanya taasisi yao iwe
kioo cha elimu wilayani Mwanga na Tanzania kwa ujumla.
“Taasisi
inaendelea kutoa elimu bora kwa kuweka miundo mbinu mizuri katika shule zake za
sekondari na chuo pia hapa wilayani Mwanga, ambapo kwa pamoja tunasonga mbele
kutolkana na ushirikiano mkubwa tunaopata kutoka serikalini na kwa wananchi
wote,” Alisema Julysiza.
Kwa mujibu wa Julysiza, elimu inayotolewa kwenye shule
zinazomilikiwa na taasisi yao ni bora na imechangia katika uandaaji wa watoto
kwa makundi mengi ya kielimu kama vile sekondari na chuo kinachofundisha
biashara, elimu na afya.
0 comments:
Post a Comment