
KATIBU
Mkuu wa Shirika la Dawa Asilia na Ulinzi wa Mazingira
Tanzania(TRAMEPRO) Boniventura Mwalongo amekutana na kufanya mazungumzo
na Chifu Msangia Ongati Ngoje wa Rorya ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa
Machifu na Mzee wa Mila na Desturi Mkoa wa Mara.
Kikao
hicho kilijikita katika kujadili mustakabali wa taifa letu, hususan
katika maeneo ya utatuzi wa migogoro ya ardhi, maadili ya jamii,
uadilifu katika utumishi wa umma, pamoja na dira ya maendeleo ya muda
mrefu ya Tanzania.
Taarifa
ya Makamu Mwenyekiti wa Machifu na Mzee wa Mila na Desturi Mkoa wa Mara
Chifu Msangia Ongati Ngoje amesema katika kikao hicho, wamekubaliana
kuimarisha nafasi ya mila na desturi katika utatuzi wa migogoro ya
ardhi, kurejesha na kuendeleza maadili na uadilifu katika jamii na
taasisi za umma.
Pia
kujenga taifa lenye umoja, uwajibikaji na matumizi bora ya rasilimali.
Aidha, walisisitiza umuhimu wa kuendeleza sekta ya tiba asili kama
nyenzo ya afya na uchumi, na kulinda pamoja na kuendeleza utamaduni wa
Waluo kama urithi muhimu wa taifa.
Amesena
kama alivyosema mwanafalsafa mashuhuri William Shakespeare, “Ujinga ni
laana; maarifa ni mabawa yanayotuinua juu.” ambapo nukuu hiyo
inatukumbusha umuhimu wa sayansi, maarifa na elimu katika kuleta
maendeleo endelevu ya jamii.
Pia
amesema, “Mguso mmoja wa asili huwafanya watu wote kuwa ndugu,”
akisisitiza nafasi ya mazingira katika kuunganisha binadamu wote.
Aidha,
katika kuelezea maisha ya jamii na utamaduni wake, alisema, “Maisha
yetu yamefumwa kwa nyuzi mchanganyiko—mema na mabaya pamoja,” jambo
linalotukumbusha wajibu wa kuhifadhi mema ya utamaduni wetu na
kurekebisha kasoro zilizopo.
Kwa
upande wa uongozi wa kitaifa, amesema Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan,
amewahi kusisitiza kuwa, “Mila na desturi zetu ni utambulisho wetu kama
taifa, ni wajibu wetu kuzilinda, kuziheshimu na kuzitumia kama chachu ya
maendeleo endelevu.”
Kauli hiyo inaonesha dhamira ya serikali katika kuendeleza urithi wa kitamaduni sambamba na maendeleo ya kisasa.
Kwa
upande wa maendeleo ya eneo, Shirati ni Halmashauri ya Mji Mdogo
iliyopo katika Wilaya ya Rorya, Mkoa wa Mara, Kaskazini mwa Tanzania,
karibu na mpaka wa Kenya na kandokando ya Ziwa Victoria.
“Mji
huu unakadiriwa kuwa na wakazi kati ya 50,000 hadi 100,000, huku Wilaya
ya Rorya ikiwa na takribani wakazi 354,490 kwa mujibu wa Sensa ya mwaka
2022. Idadi kubwa ya wakazi ni vijana wanaoishi vijijini.
“Shughuli
kuu za kiuchumi katika eneo hili ni pamoja na kilimo kinachotegemewa na
zaidi ya asilimia 80 ya wananchi, kikijumuisha mazao ya mahindi,
mihogo, mtama, alizeti na pamba.
“Uvuvi
pia ni shughuli muhimu inayofanyika katika Ziwa Victoria ukihusisha
samaki kama sangara, sato na dagaa. Aidha, wananchi hujihusisha na
ufugaji wa ng’ombe, mbuzi na kondoo pamoja na biashara ndogo ndogo,
ikiwemo biashara za mipakani kati ya Tanzania na Kenya.”
Amesema
Kijiografia, eneo la Shirati liko katika Mkoa wa Mara, kaskazini mwa
Tanzania, karibu na mpaka wa Kenya na kuzungukwa na Ziwa Victoria,
likiwa na hali ya hewa ya kitropiki yenye mvua za msimu. Hali hii
huchangia kwa kiasi kikubwa shughuli za kiuchumi na maisha ya wananchi
wa eneo hilo.
Amesema
utamaduni wa Waluo unaendelea kuwa nguzo muhimu ya mshikamano wa jamii,
ukijengwa juu ya heshima kwa wazee na viongozi wa mila, matumizi ya
baraza la wazee katika utatuzi wa migogoro, mshikamano wa kifamilia na
kijamii, pamoja na kuzingatia maadili ya uadilifu, uwajibikaji na
upendo.
Pamoja
na hayo amesema ni wazi ushirikiano kati ya viongozi wa mila na
desturi, serikali, wataalamu na wananchi ni muhimu katika kujenga jamii
yenye maadili imara, uchumi thabiti na maendeleo endelevu.
“Tunatoa
mwito kwa wadau wote kushiriki kikamilifu katika kulinda mazingira,
kuendeleza tiba asili, kuhifadhi utamaduni wa Waluo na kutumia vyema
fursa zilizopo kwa maendeleo ya Mkoa wa Mara na taifa kwa
ujumla,”amesema Chifu Msangia Ongati Ngoje wa Rorya.
.jpeg)

0 comments:
Post a Comment