Na Mwandishi Wetu - Dar es Salaam
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe. Balozi Dkt. Batilda Burian ametoa wito kwa wananchi kuendelea kujitokeza kupata elimu ya masuala mbalimbali katika Banda Jumuishi la Ofisi ya Waziri Mkuu na Taasisi zake katika Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba 2026) yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.
Ametoa wito huo hii leo (12 Julai, 2026)
alipotembelea na kujionea namna ofisi hiyo inavyoendelea kutoa huduma kwa wananchi na kuwasihi waendelee kujitokeza kwa wingi na kupata taarifa na huduma zinazotolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu pamoja na taasisi zake.
Dkt. Batilda amepongeza namna Ofisi ya Waziri Mkuu ilivyojipanga na kuhakikisha inawafikia wananchi kwa utoaji wa huduma bora na kuzingatia viwango huku wakiendelea kutatua changamoto mbalimbali kwa jamii kupitia maonesho hayo.
Aidha amewakumbusha watumishi wa ofisi hiyo kuendelea kuwa na program mbalimbali za elimu kwa umma ili kuifikia jamii kwa ukumbwa wake na kuendelea kutangaza huduma zinazotolewa.
Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam yanaendelea katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere chini ya kaulimbiu isemayo, "Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba ni Fahari ya Tanzania," yakilenga kukuza biashara, uwekezaji na ubunifu, nchini.







0 comments:
Post a Comment