
Na Mwandishi Wetu, Manyara
Mbio hizo zilizoendeshwa chini ya kaulimbiu “Hatua Moja, Okoa Maisha ya Mtoto Njiti”, zimewakutanisha wananchi, wanariadha na wadau mbalimbali kutoka maeneo tofauti nchini, kwa lengo la kuunga mkono juhudi za kuboresha huduma za afya kwa watoto wachanga na watoto njiti.
Mgeni rasmi kwa niaba ya Waziri Mkuu, Mhe. Mwigulu Nchemba, ambaye ni Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Daniel Sillo, amepongeza Mkoa wa Manyara kwa kuanzisha mbio hizo, akisema ni ubunifu unaolenga kushirikisha jamii katika kuchangia huduma za afya.
Sillo amesema Manyara Tanzanite Marathon ni mfano wa namna matukio ya michezo yanavyoweza kutumika katika kuhamasisha jamii na wadau kuchangia miradi yenye manufaa kwa wananchi, hususan katika sekta ya afya.
Amesema jitihada hizo zinapaswa kuungwa mkono na maeneo mengine nchini ili kuongeza ushiriki wa jamii katika kutatua changamoto zinazowakabili wananchi.
MBIO
za hisani za Manyara Tanzanite Marathon 2026 zimefanyika leo katika Mji
wa Babati, mkoani Manyara, huku waandaaji wakiwa na lengo la kukusanya
Sh1.5 bilioni kwa ajili ya ujenzi na uwezeshaji wa wodi maalum ya
kuwahudumia watoto wanaozaliwa kabla ya wakati.
Mgeni rasmi kwa niaba ya Waziri Mkuu, Mhe. Mwigulu Nchemba, ambaye ni Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Daniel Sillo, amepongeza Mkoa wa Manyara kwa kuanzisha mbio hizo, akisema ni ubunifu unaolenga kushirikisha jamii katika kuchangia huduma za afya.
Sillo
amesema Manyara Tanzanite Marathon ni mfano wa namna matukio ya michezo
yanavyoweza kutumika katika kuhamasisha jamii na wadau kuchangia miradi
yenye manufaa kwa wananchi, hususan katika sekta ya afya.
Amesema
jitihada hizo zinapaswa kuungwa mkono na maeneo mengine nchini ili
kuongeza ushiriki wa jamii katika kutatua changamoto zinazowakabili
wananchi.
Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Queen Sendiga, amewashukuru wadau walioshiriki katika maandalizi na utekelezaji wa mbio hizo, akisema ushirikiano wao umewezesha kufanikisha tukio hilo lenye lengo la kuchangisha fedha kwa ajili ya watoto wanaohitaji huduma maalumu za afya.
Sendiga
amesema fedha zitakazopatikana kupitia mbio hizo zitaelekezwa katika
kufanikisha ujenzi na uwezeshaji wa wodi maalum kwa ajili ya kuwahudumia
watoto njiti, ambao huhitaji huduma za kitaalamu na vifaa maalumu tangu
wanapozaliwa.
Wamesema Manyara Tanzanite Marathon imewapa fursa ya kuunganisha michezo na shughuli za kijamii, huku wakitoa wito kwa wananchi wengine kushiriki katika matukio yenye malengo ya kuboresha afya na ustawi wa jamii.
Manyara Tanzanite Marathon 2026 imeweka lengo la kukusanya Sh1.5 bilioni, ikiwa ni sehemu ya kampeni ya “Hatua Moja, Okoa Maisha ya Mtoto Njiti” inayolenga kuongeza uwezo wa huduma za afya kwa watoto wanaozaliwa kabla ya wakati mkoani Manyara.





































0 comments:
Post a Comment