Waelimishaji kutoka Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi (SSRA), wakiwa katika picha ya pamoja na
wadau wa Chuo cha Ualimu Matogoro, Songea, mkoani Ruvuma, wakati mamlaka hiyo, ilipokuwa ikitoa elimu kwa umma hivi karibuni.
Baadhi ya wakulima wa Mkoa wa Ruvuma wakifuatilia mada ya
Hifadhi ya Jamii kutoka SSRA wakati wa semina za elimu kwa umma zilizoendeshwa na
Mamlaka hiyo.
Mkuu Kitengo cha Ununuzi wa SSRA, Bw. Emmanuel Urembo, akitoa
mada kwa wanafunzi wa Chuo cha Ufundi Stadi (VETA) Mjini Songea.
Wakulima wa Mkoa wa Njombe, wakisikiliza mada kuhusu Hifadhi
ya Jamii kutoka kwa waelimishaji wa SSRA, wakati wa semina za elimu kwa umma zilizoendeshwa na SSRA mkoani humo hivi karibuni.
Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Uhamasishaji wa SSRA, Bi. Saraha Kibonde Msika, akitoa ufafanuzi kuhusu masuala mbalimbali ya Hifadhi ya
Jamii kwa wanafunzi wa Chuo cha Ufundi Stadi (VETA), Makete hivi karibuni.
Waelimishaji kutoka SSRA, Bi. Sarah Kibonde Msika (katikati) na Bw. David
Lyanga (kulia mbele), wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Chuo cha Ualimu Hagafilo
Njombe.
Ofisa kutoka SSRA, Bw. David Lyanga akitoa mada kuhusu
Hifadhi ya Jamii wakati wa semina za elimu kwa umma zilizoendeshwa na SSRA, mkoani Njombe hivi karibuni.
Waelimishaji kutoka SSRA, Bi. Sarah
Kibonde Msika (katikati) na Bw David Lyanga (wa pili kushoto), wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi
na wanafunzi wa Chuo cha Ufundi Stadi (VETA) Makete, mkoani Njombe hivi karibuni.
Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa SSRA, Bw. Peter Mbelwa akitoa maelezo kuhusu
masuala ya Hifadhi ya Jamii wakati wa Semina iliyoandaliwa na Mamlaka ya
Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), iliyofanyika kwa
Wanachuo na Wafanyakazi wa Chuo cha
Ufundi Binza, kilichopo Wilaya ya Maswa, mkoani Simiyu hivi karibuni.
Ofisa uhusiano wa Mamlaka ya
Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Bi. Agnes Lubuva
akitoa mada ya Hifadhi ya Jamii kwa wanafunzi na wafanyakazi wa Chuo cha Ufundi
Binza kilichopo Wilaya ya Maswa, mkoani Simiyu, hivi karibuni.
Wafanyakazi wa SSRA wakiwa katika picha ya pamoja na Wanachama wa
Mtandao wa vikundi vya Wakulima
(MVIWATA), baada ya kupata Semina ya Hifadhi ya Jamii iliyofanyika Bariadi, Kata
ya Lugulu, hivi karibui. (Picha zote na SSRA).
0 comments:
Post a Comment