Waziri wa Elimu Dkt.Shukuru Kawambwa akitoa tuzo maalum kwa Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kwa kutambua mchango wake katika kuendeleza na kuboresha elimu nchini wakati wa maadhimisho ya kilele cha wiki ya elimu yaliyofanyika katika uwanja wa michezo wa Jamhuri mjini Dodoma leo.
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimpa zawadi mwanafunzi Agatha Julius Ninga
kutoka Shule ya sekondari ya wasichana ya Tabora akiwa ni miongoni mwa
wanafunzi sita waliofaulu vizuri katika mitihani ya sayansi ya kidato
cha nne mwaka jana 2014.Agatha alifanya vizuri katika somo la
Biolojia.Rais Kikwete alitoa zawadi kwa wanafunzi, shule,halmashauri na
mikoa iliyofanya vizuri na kuongeza ufaulu katika mitihani ya Taifa
kumaliza Elimu ya msingi na elimu ya sekondari.Tuzo na zawadi hizo
zilitolewa leo katika uwanja wa michezo wa Jamhuri mjini Dodoma wakati
wa maadhimisho ya kilele cha wiki ya elimu nchini.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akitoa hotuba yake wakati wa maadhimisho ya kilele cha Wiki ya Elimu kitaifa iliyofanyika mjini Dodoma leo.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiangalia wanafunzi Maria Sagasii na Neema Harry kutoka Shule ya msingi ya Ignatius ya mjini Dodoma wakionyesha viungo vya ndani vya mwili wa binadamu somo la Biolojia katia banda la maonyesho katika Uwanja wa michezi wa Jamhuri wa mjini Dodoma wakati wa kilele cha maadhimisho ya Wiki ya Elimu leo.
Baadhi ya Wanafunzi kutoka katika shule mbalimbali mjini Dodoma waliohudhuria sherehe za kilele cha wiki ya Elimu kitaifa zilizofanyika katika uwanja wa michezo wa Jamhuri mjini Dodoma Mei 15,2015 .PICHA ZA FREDDY MARO, IKULU.
0 comments:
Post a Comment