Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Cheki ya Sh. Milioni 3, mshindi wa kwanza wa Mashindano ya Tano ya kuhifadhi Qur-an Tukufu, Said Nassor Said, aliyehifadhi Juzuu 30, wakati wa hafla fupi ya Utoaji wa Tuzo na Kuwakirimu washindi hao wa mashindano yaliyoandaliwa na
Taasisi ya Istiqaama. Hafla hiyo ilifanyika kwenye Msikiti wa Istiqaama Ilala
jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na waumini wa dini ya Kiislamu wakati wa hafla fupi ya Utoaji wa Tuzo na Kuwakirimu washindi wa Mashindano ya Tano ya kuhifadhi Qur-an Tukufu yaliyoandaliwa na Taasisi ya Istiqaama, iliyofanyika
kwenye Msikiti wa Istiqaam, Ilala jijini Dar es Salaam jana usiku.
Sehemu ya waumini wa Dini ya Kiislamu waliohudhuria hafla hiyo.
Dkt. Bilal, akikabidhiwa Tuzo ya Heshima kwa kutambua mchango wake katika kufanikisha elimu ya Qur -an.
Dkt. Bilal, akionyesha Tuzo yake...
Mshindi wa Juzuu 30, akisoma moja ya sura
Mmoja kati ya washindi wa mashindano hayo, akisoma
Waumini wakiomba Dua...
Mmoja kati ya washindi akipongezwa na Dkt. Bilal, baada ya kutangazwa..
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Balozi wa Iran nchini Tanzania, Mehdi Aghajafari, wakati akiondoka kwenye Msikiti wa Istiqaama jana usiku baada ya kushiriki swala ya Talaweh nukabidhi Tuzo za Kuwakirimu washindi wa Mashindano ya Tano ya kuhifadhi Qur-an
Tukufu yaliyoandaliwa na Taasisi ya Istiqaama.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya Waumini wa Dini ya Kiislamu wakati akiondoka kwenye Msikiti wa Istiqaama jana usiku baada ya kushiriki swala ya Talaweh na kukabidhi Tuzo za Kuwakirimu washindi wa Mashindano ya Tano ya kuhifadhi Qur-an Tukufu yaliyoandaliwa na Taasisi ya Istiqaama
0 comments:
Post a Comment