Balozi wa Ireland nchini Tanzania, Bi. Fionnuala Gilsenan, akizungumzia kuhusu ufadhili kwa Watanzania wanaokwenda vyuo mbalimbali vya ndani na nje ya nchi. Sherehe hizo zimefanyika Alhamisi, Agosti 20, 2015 kwenye ofisi za ubalozi huo Masaki jijini Dar es Salaam. (Picha na habari na Daniel Mbega wa www.brotherdanny.com).
Baadhi ya wanufaika wa ufadhili huo wakimsikiliza Balozi wa Ireland (hayuko pichani).
Baadhi ya wafanyakazi na wageni waalikwa wakimsikiliza Balozi Gilsenan.
Deogratias Gabriel Rugarabamu, Ofisa Tabibu wa Wilaya ya Kilindi, akipokea cheti cha shukrani baada ya kuhitimu shahada ya uzamili ya Medical Entomology and Clinical Parasitology katika Chuo Kikuu cha Tumaini, KCMC .
Balozi Fionnuala Gilsenan wa Ireland akimpongeza Rubea Mohammed Ali, Mkuu wa Idara katika Wizara ya Kilimo na Maliasili, Zanzibar baada ya kuhitimu shahada ya uzamili katika Chuo Kikuu cha Sokoine katika Elimu ya Kilimo na Ushauri (Agricultural Education and Extension).
David Eliatosha Lekei, Ofisa Kilimo Wilaya ya Hai akipokea cheti cha shukrani kutoka kwa Balozi wa Ireland nchini, Bi.Fionnuala Gilsenan baada ya kuhitimu shahada ya uzamili kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine katika Elimu ya Kilimo na Ushauri (Agricultural Education and Extension).
Mshereheshaji akisoma majina ya wanufaika.
Stella Zakayo Munisi, Meneja Rasilimali Watu na Utawala wa Shirika la Sikika, akipokea hati ya ufadhili kwenda kusomea shahada ya uzamili kuhusu Organizational Development and Change katika Chuo Kikuu cha Dublin, Ireland.
Na Daniel Mbega.
SERIKALI
ya Ireland kupitia Ubalozi wake nchini Tanzania, leo Agosti 20, 2015 imekabidhi scholarship
kwa Watanzania 14 ambao watakwenda kusomea kozi mbalimbali za shahada ya
uzamili (masters) ambapo wanne kati yao wakienda kusoma vyuo vikuu nchini
Ireland.
Akikabidhi
hati hizo za ufadhili wa masomo, Balozi wa Ireland nchini Tanzania, Bi. Fionnuala
Gilsenan, alisema utaratibu wa kutoa ufadhili kwa wataalamu mbalimbali ni jambo
la msingi kutokana na ukweli kwamba ujuzi watakaoupata unaweza kuliletea taifa
maendeleo.
“Ufadhili
huu ni sehemu ya Mpango wa Mafunzo wa Kila Mwaka (Fellowship Training
Programme), katika sukuma mbele maendeleo ya nchi washirika wetu, tunadhani
tunao wajibu wa kusaidia pia kuwaelimisha watalaamu wao,” alisema.
Aliwataja wanufaika
wanne waliobahatika kwenda ng’ambo kuwa ni Stella Zakayo Munisi, Meneja
Rasilimali Watu na Utawala wa Shirika la Sikika, ambaye anakwenda kusomea
shahada ya uzamili (Organizational Development and Change) na Cosmas Joseph
Mworia, Ofisa Ushirika na Ofisa Ufuatiliaji na Ukadiriaji katika Kilimo wa
Halmashauri ya Wilaya Kondoa anayekwenda kusomea shahada ya uzamili katika
Kilimo Endelevu na Maendeleo Vijijini (Sustainable Agriculture and Rural
Development). Wawili hao wanakwenda katika Chuo Kikuu cha Dublin.
Flavian
Majenga Lihwa, Mratibu Programu ya Elimu wa Shirika la Care Tanzania yeye
anakwenda Chuo Kikuu cha Dublin Institute of Technology kuchukua shahada ya
uzamili katika Maendeleo Endelevu (Sustainable Development) na Zabron Elias
Masatu, Mganga Mkuu wa Wilaya (DMO) ya Misenyi yeye anakwenda Chuo Kikuu cha
Taifa cha Ireland Maynooth (NUIM) kuchukua shahada ya uzamili ya Immunolojia na
Afya (Immunology and Global Health).
Wanufaika
wengine 10 wa mwaka huu, kozi na vyuo wanavyokwenda vikiwa kwenye mabano ni, Siwajibu
Ally Selemani Malenge, Kaimu Ofisa Kilimo/Umwagiliaji na Ushirika wa Wilaya ya
Kigoma (Chuo Kikuu cha Sokoine – Elimu ya Kilimo na Ushauri ‘Agricultural
Education and Extension’); Edita Byangwamu Rutatora Kokwijuka, Ofisa Kilimo
Daraja la Kwanza kutoka Wilaya ya Muheza (Chuo Kikuu cha Sokoine – Kilimo); Doreen
Elias Mangesho, Mhasibu Mkuu wa CCBRT (Chuo Kikuu cha Dar es Salaam – Utawala wa
Fedha); Elinlaa Michael Kivaya, Mchumi wa Kilimo wa Wilaya ya Ngorongoro (Chuo
Kikuu cha Sokoine – Kilimo na Uchumi Mtambuka ‘Agriculture and Applied Economics’);
na Joshua Julius Musimu, Mkufunzi wa Kilimo Daraja la Pili kutoka Wizara ya
Kilimo, Chakula na Ushirika (Chuo Kikuu cha Sokoine – Uchumi wa Kilimo ‘Agricultural
Economics’).
Wengine ni
Fredrick Pius Massawe, Ofisa Kilimo Daraja la Kwanza kutoka Ofisi ya Katibu
Tawala Mkoa wa Kilimanjaro (Chuo Kikuu cha Sokoine –Kilimo); Samuel Korinja
Olekao, Mratibu wa Kinnapa Development Programme (Chuo Kikuu cha Sokoine – Utunzaji
wa Maliasili na Kilimo Endelevu); Eva Emmanuel Mbambale, Ofisa Program wa
Sikika (Chuo Kikuu cha Makerere,Uganda – Afya ya Jamii); Iddi Alfani Shekabugi,
Mchumi Daraja la Kwanza katika Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika (Chuo
Kikuu cha Mzumbe – Uchumi na Fedha kwa Maendeleo); na Felix Lyope Lubuga, Ofisa
Utafiti wa Taasisi ya Afya Ifakara (Chuo Kikuu cha Dar es Salaam – Afya ya
Jamii).
Awali,
Balozi Fionnuala aliwatunuku vyeti wanufaika wengine 10 waliomaliza mwaka 2013
na 2014 katika fani mbalimbali.
0 comments:
Post a Comment