Vijana kutoka vikundi mbalimbali wakitoa
burudani wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya vijana duniani katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam Agosti 12, 2015
Mwakilishi
Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia idadi ya watu duniani
(UNFPA) Bibi. Natalia Kanem akizungumza na vijana wakati wa Maadhimisho ya siku
ya kimataifa ya vijana duniani leo katika Viwanja vya Mnazi Mmoja. Kushoto ni
Mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo
Prof. Elisante Ole Gabriel
Kijana
ambaye ni mwanachama wa asasi ya vijana chini ya umoja wa mataifa (YUNA) Bw.
Hesein Melele akiwasilisha maazimio yaliyofikiwa na vijana wakati wa kongamano
lililofanyika Agosti 10 mwaka huu kujadili ujumbe wa siku ya kimataifa ya vijana
duniani na kuandaa maazimio yaliyowasilishwa kwa mgeni rasmi leo katika Viwanja
vya Mnazi Mmoja walipokua wakiadhimisha siku ya kimataifa ya vijana duniani.
Naibu
Katibu Mkuu kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof.
Elisante Ole Gabriel (kushoto) akiwahutubia vijana walioshiriki maadhimisho ya
siku ya kimataifa ya vijana duniani leo katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini
Dar es Salaam. Kulia ni Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa
linaloshughulikia idadi ya watu duniani (UNFPA) Bibi. Natalia Kanem.
Baadhi
ya vijana wakifuatilia kwa makini matukio mbalimbali yaliyokua yakiendelea
wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya vijana duniani leo katika Viwanja
vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Naibu
Katibu Mkuu kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof.
Elisante Ole Gabriel (kushoto) akisikiliza kwa makini maelezo kutoka kwa Afisa
Vijana Bi. Amina Sanga (kulia) alipotembelea banda la Wizara ya Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya vijana
duniani yaliyoadhimishwa leo katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es
Salaam. Wapili kulia ni Mkurugenzi Maendeleo ya Vijana Bw. James Kajugusi.
Baadhi ya vijana kutoka shule mbalimbali
wakiandamana kuingia katika viwanja vya mnazi mmoja wakati wa maadhimisho ya
siku ya kimataifa ya vijana duniani iliyoadhimishwa leo jijini Dar es Salaam na
kuhusisha mashirika mbalimbali ya mataifa yanayofanya shughuli za vijana
yakiwemo UNFPA, IYF, UNIC, ILO, RESTLESS DEVELOPMENT, YUNA, AMREF, MARIE
STOPES, pamoja na PSI.
Mgeni
rasmi Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof.
Elisante Ole Gabriel (wapili kulia) akipokea maandamano ya vijana (hawapo
pichani) wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya vijana duniani iliyoadhimishwa
katika Viwanja vya Mnazi Mmoja leo jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kushoto ni
Mkurugenzi Maendeleo ya Vijana Bw. James Kajugusi na wapili kushoto ni
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia idadi ya watu
duniani (UNFPA) Bibi. Natalia Kanem.
0 comments:
Post a Comment