Balozi
wa China nchini Tanzania, Dk.Lu Youqing (katikati), akihutubia wakati
akizindua kampeni ya kupambana na ujangili viwanja vya Leaders Club Dar
es Salaam leo asubuhi. Kampeni hiyo imeanzishwa na watu wa China kwa
ajili ya kuunga jitihada za watanzania katika mapambano hayo ya
kuwalinda wanyama dhidi ya ujangili hasa tembo.
Balozi
wa China nchini Tanzania, Dk.Lu Youqing (kulia), akimpa zawadi ya mpira
kwa niaba ya wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Kinondoni, Faudhia Eddy
katika uzinduzi huo. Balozi huyo alitoa zawadi ya mipira kwa baadhi ya
shule za Manispaa ya Kinondoni.
Balozi
wa China nchini Tanzania, Dk.Lu Youqing (kulia), akimpa zawadi ya
mpira, Mwalimu Flora Lukali kutoka Shule ya Mount Pleasant kwa ajili ya
shule hiyo.
Balozi wa China nchini Tanzania, Dk.Lu
Youqing akionyesha umahiri wa kuchezea mpira katika uzinduzi huo kabla
ya kutoa zawadi ya mipira kwa baadhi ya shule za Manispaa ya Kinondoni.
Wanafunzi wakiwa na vipeperushi vya bendera ya nchi ya china wakati wa uzinduzi huo.
Wasanii wa kundi la makhirikhiri wakitoa burudani katika
uzinduzi huo.
Wanafunzi wakiwa kwenye uzinduzi huo.
Wimbo wa taifa ukiimbwa.
Wanahabari wakichukua taarifa za uzinduzi huo.
Wanafunzi ndani ya uzinduzi huo.
0 comments:
Post a Comment