Mtalaam wa masuala ya Biogesi na Majiko Sanifu wa
Taasisi ya kuendeleza Nishati Asilia na Uhifadhi wa Mazingira Tanzania (
TaTEDO) Bw.Stephen Boniface akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari
kuhusu ujenzi wa mtambo wenye uwezo wa kuzalisha gesi yenye mita za
ujazo 200 walioujenga katika shule ya Sekondari Manzese iliyoko
wilayani Kinondoni jijini Dar es Salaam jana. Kulia kwake ni Mkuu wa
Shule ya Sekondari Manzese Bw.Linus Mwakasege.
Meneja Uhusiano wa Jamii wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar
es salaam (DAWASA) Bi.Neli Msuya akielezea ushiriki wa DAWASA katika
kufanikisha ujenzi wa Mradi wa Biogesi katika shule ya Sekondari Manzese
ya jijini Dar es salaam mara baada ya kutembelea mradi huo jana jijini
Dar es salaam.
Mkuu wa Shule ya
Sekondari Manzese Bw.Linus Mwakasege akitoa ufafanusi kwa waandishi wa
habari kuhusu manufaa ya mradi wa nishati endelevu ya Biogesi
utakavyowanufaisha wanafunzi wa shule hiyo.
Mtaalam wa Nishati Endelevu na mabadiko ya Tabia nchi Bw. Shima
Sango kutoka Taasisi ya Uendelezaji wa Nishati asilia na Uhifadhi wa
Mazingira (TaTEDO) Akiwasha moja ya jiko la gesi liliojengwa katika
shule ya Sekondari Manzese.
Picha na Aron Msigwa - MAELEZO.
---
---
SHULE
za Sekondari kote nchini zimeshauriwa kuwekeza katika matumizi ya
Nishati endelevu ya Biogesi na majiko sanifu ili kulinda na kuhifadhi
mazingira.
Ushauri huo umetolewa na Meneja
Uhusiano wa Jamii wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es salaam
(DAWASA) Bi.Neli Msuya mara baada ya kutembelea ujenzi wa Mradi wa
kuzalisha Nishati endelevu ya Biogesi katika Shule ya Sekondari
Manzese wilayani Kinondoni, jijini Dar.
0 comments:
Post a Comment