Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Mhandisi Stella Manyanya (wa pili kulia) akikata utepe na Makamu wa Rais wa Kampuni ya Total, Jean-Christian Bergeron (wa tatu kulia) wakati wa hafla ya kukabidhi madawati 1000 yaliyotolewa kama msaada na Total kwa ajili ya Shule 10 za mikoa ya Dar es Salaam na Pwani. Makabidhiano hayo yalifanyika wilayani Bagamoyo jana. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Prof. Naomi Katunzi (kulia) na Kushoto anayeshuhudia ni mwanafunzi wa shule ya msingi Nianjema ya Bagamoyo, Ramadhani Issa. (Picha na Francis Dande)
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Mhandisi Stella Manyanya (kushoto) akimshukuru Makamu wa Rais wa Kampuni ya Total, Jean-Christian Bergeron baada ya kupokea sehemu ya msaada wa madawati 1000 yaliyotolewa na kampuni hiyo kwa ajili ya Shule 10 za mikoa ya Dar es Salaam na Pwani. Makabidhiano hayo yalifanyika wilayani Bagamoyo jana. Katikati ni mwanafunzi wa shule ya msingi Nianjema, Ramadhan Hassan.
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Mhandisi Stella Manyanya (kushoto) akiwa amekaa katika madawati yaliyotolewa kama msaada na Kampuni ya Total. Katikati ni Makamu wa Rais wa Kampuni ya Total, Jean-Christian Bergeron, madawati 1000 yaliyotolewa na kampuni hiyo yakiwa na thamani ya shs. milioni 78 kwa ajili ya Shule 10 za mikoa ya Dar es Salaam na Pwani. Wa pili kushoto ni mwanafunzi wa shule ya msingi Nianjema ya Bagamoyo, Ramadhani Issa.
0 comments:
Post a Comment