Mwalimu wa watoto wenye Usonji shule ya msingi Makumbusho Bi. Kuluthumu Samatha akionesha namna watoto wenye ulemavu huo wanavyosalimia wakati wa ziara ya Naibu Waziri (Watu wenye Ulemavu) Mhe. Dkt. Abdallah Possi (hayupo pichani) shuleni hapo Februari 29, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Mwalimu wa watoto wenye Usonji shule ya msingi Makumbusho Bi. Azizi Issa akitoa neno la shukrani kwa Naibu Waziri (Watu wenye Ulemavu) Mhe. Dkt. Abdallah Possi (wa kwanza kulia) wakati wa ziara yake alipotembelea shule na vituo vinavyolea watoto wenye ulemavu na mahitaji maalum mkoani Arusha Februari 29, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Naibu Waziri (Watu wenye Ulemavu) Mhe. Dkt. Abdallah Possi akiangalia vifaa vya michezo vya watoto wenye Usonji (bembea) wanazozitumia wakati wa mapumziko ikiwa ni sehemu ya mazoezi kwao wakati wa ziara yake mkoani Arusha Februari 29, 2016 (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Naibu Waziri (Watu wenye Ulemavu) Mhe. Dkt. Abdallah Possi (wa tano kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya walimu wa shule ya msingi Meru pamoja na baadhi ya viongozi kutoa Wilaya ya Arusha mjini, wakati wa ziara ya kutembelea Shule, vyuo na vituo vya kulea watu wenye ulemavu Arusha. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Naibu Waziri (Watu wenye Ulemavu) Mhe. Dkt. Abdallah Possi akizungumza na watoto wenye ulemavu wa ngozi (albinism) katika ziara yake shule ya Arusha ikiwa ni moja ya kituo alichotembelea mkoani Arusha Februari 29, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Naibu Waziri (Watu wenye Ulemavu) Mhe. Dkt. Abdallah Possi akisalimiana na baadhi ya walimu wa shule ya msingi Arusha wakati wa ziara yake ya kuangalia hali ilivyo katika Vituo, Vyuo na shule zinazolea watoto wenye ulemavu Mkoani Arusha. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Naibu Waziri (Watu wenye Ulemavu) Mhe. Dkt. Abdallah Possi akisalimiana na mwanafunzi wa shule ya msingi Themi mwenye tatizo la uoni Bi. Lissa Lucas wakati wa ziara yake shuleni hapo Februari 29, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Naibu Waziri (Watu wenye Ulemavu) Mhe. Dkt. Abdallah Possi akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari ya Longido mkoani Arusha wakati wa ziara ya kutembelea watoto wenye ulemavu na mahitaji maalum mkoani hapo Februari 29, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
0 comments:
Post a Comment