.Oh "Kumbe kinafanya kazi hivi" ndivyo anavyoelekea kusema Rais
Obama mara baada ya kuweza kukiendesha kifaa hicho kwa kutumia simu,
aliyechuchuma ni Stephen Mwingira ambaye pamoja na Wendy Ni na Armon
Halwan walipata fursa ya kuonyesha ubunifu wao katika onyesho la mwisho
lililoandaliwa na Rais Barack Obana na kufanyika White House April
13. 2016.
.Mwanafunzi Armo Halwan akimuelekeza Rais wa Marekani,Barack Obama
anavyoweza kutumia simu kuendesha cha kufanyia usafi ( Vacuum
Cleaner) kilichobuniwa na wanafunzi wa Baruch Collage Campus High School
ya Jijini New York kupitia timu yao ya ufumbuzi (Invent Teams)katikati
ni Wendy Ni na anayefuatia ni Stephen Mwingira ( mtanzania) anaonyesha
namna gani kifaa hicho kinavyofanya usafi kwenye njia za treni za
ardhini ( Subways).
Stephen Mwingira na Wendy Ni, wakiangalia kwa makini jinsi Rais Obama
anavyoelekezwa namna ya kutumia simu kuendesha mashine hiyo katika
Onyesho la ubunifu wa kisayansi ambalo lilifadhiliwa na Rais Barack
Obama katika Ikulu ya Rais ( White House Science Fair 2016)
Rais Barack Obama akipeana mkono na Stephen Mwingira na timu yake
baada ya kumaliza kutoa maelezo yao kifaa walichokibuni. Kwa miaka sita
Rais Barack Obama amekuwa akifadhili maonyesho ya ubunifu wa vifaa
mbalimbali vilivyobuniwa na wanafunzi kuanzia wale wa shule za wali
hadi sekondari ikiwa ni jitihada zake za kuwahamasisha wanafunzi
kupenda masomo ya sayansi, teknolojia na hesabu tangu wakiwa wadogo na
hivyo kuibua vipaji vyao. katika onyesho hilo la mwisho wa utawala wa
Barack Obama jumla ya wanafunzi 130 kutoka states mbalimbali
walishiriki.
Stephen Mwingira akiendelea kutoa maelezo zaidi kwa Rais Obama namna
kifanya cha kufanyia usafi kwenye njia za reli ambacho ni cha gharama
nafuu kinavyofanya kazi.
---
Rais wa Marekani, Barack Obama, alifadhili onyesho la mwisho katika utawala wake, onyesho lililohusu ubunifu katika Nyanja za sayansi ambalo limewahusisha wanafunzi kuanzia shule za awali,msingi hadi za sekondari kutoka States mbalimbali za Marekani.
---
Rais wa Marekani, Barack Obama, alifadhili onyesho la mwisho katika utawala wake, onyesho lililohusu ubunifu katika Nyanja za sayansi ambalo limewahusisha wanafunzi kuanzia shule za awali,msingi hadi za sekondari kutoka States mbalimbali za Marekani.
Kwa miaka sita tangu mwaka 2010, Kiongozi huyo wa Marekani
amekuwa akifadhili onyesho hilo lijulikanalo
kama White House Science Fair
ambalo limekuwa likifanyia katika
Ikulu yake (White House) lengo
likiwa ni kuhamasisha wanafunzi kupenda
masomo ya sayansi, hisabati ,teknolojia na
ufundi ( STEM)na hivyo kuibua
vipaji vya ubunifu
mwiongoni mwa wanafunzi ( young
inventors) .
Katika
onyesho hilo la
Aprili 13 jumla ya wanafunzi 130 walishiriki baada ya kukidhi vigezo
vya
kuingia katika onyesho hilo. Miongoni
mwa wanafunzi waliopata fursa hiyo
adhimu ya kushiriki baada ya kukidhi vigezo ya ubunifu wao ni
mwanafunzi mtanzania Stephen Wilfred Mwingira ambaye pamoja na
wenzake wawili Armo Halwah na Wendy Ni
wanaosoma Baruch College Campus High School ya jijini New York,
wamebuni kifaa cha gharama nafuu ( vacuum cleaner)
kinachoweza kutumika katika kusafisha
njia za reli za chini ya ardhi ( Subways).
Stephen Mwingira na timu yake, walipata fursa ya kuelezea na
kuonyesha mbele ya Rais Obama namna gani kifaa walichobuni ( Vacuum Cleaner) kinavyoweza kufanya usafi
kwa kufungwa kwenye treni na hivyo kusaidia katika
kuzifanya njia za treni ( subways) kuwa katika mazingira ya usafi na hivyo kupunguza gharama za usafishaji.
Katika miaka sita tangu Rais Obama ambaye yeye binafsi
amejipambanua kama mpenzi na shabiki mkubwa wa
sayansi na ubunifu, onyesho hilo limekuwa motisha na kivutio kikubwa kwa
walimu, wanafunzi, wafadhili na
wataalamu waliobeba katika masuala ya
sayansi, teknolojia na hesabu.
Kila mwaka State
dining room ya Ikulu hugeuzwa kuwa eneo la maeonyesho ambapo
wanafunzi hujipanga na kuonesha vifaa walivyobuni au kutoa maelezo ya kisayansi ya namna ya
kutatua tatizo Fulani kwa kutumia teknolojia nafuu.
Katika kutambua mchango wa Rais Barack Obama katika kuwahamasisha
wanafunzi kupenda masomo ya sayansi,
Ikulu ya White House imetangaza kwamba Kampuni ya Oracle inayojihusisha
na masuala ya teknolojia ya Komputa katika miezi kumi na nane ijayo itawekeza
dola za kimarekani 200 milioni kwaajili ya masomo ya
sayansi ya computa kwa wanafunzi
wa kimarekani.
Katika
maelezo yake kwa vyombo vya habari kabla na baada
ya kuhitikishwa kwa onyesho lake la
mwisho, Rais Barack Obama amesema, mara
zote ambazo ameshiriki kujionea ubunifu wa vijana hao wadogo na wenye
kiu na
ari ya kuibua mambo mapya, amekuwa akijifunza kitu kipya na mara zote
amejiona kama anayepungukiwa na kitu kutokana kile anachojifunza
kutoka kwa wanafunzi hao.
“Nimeweza kujionea ubunifu
wa hali ya juu, kiu, na hamu ya
watoto na vijana wetu wataalamu
wa kesho wa taifa letu la marekani. Ipo siku huko mbeleni nitajivunia pale ambapo miongoni mwa vijana
wetu hawa watakapoweza kubuni tiba ya kansa. Nitaangalia nyuma kwa fahari kubwa kwamba niliwawezesha
vijana hawa kuibua vipaji vyao ”. Akasema Rais Obama kwa furaha huku akiwashukuru wale wote ambao kwa miaka
sita mfululizo wamewezesha kwa namna moja ama nyingine kufanyika kwa onyesho
hilo.
0 comments:
Post a Comment