Taifa Laomboleza: TRAMEPRO Yaungana na Waumini Kumkumbuka Kardinali Pengo

Shirika la TRAMEPRO limetoa salamu za rambirambi kufuatia kifo cha Mwadhama Polycarp Cardinal Pengo, Askofu Mkuu Mstaafu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, aliyefariki Februari 24, 2026.

Katika salamu hizo zilizotolewa na Katibu Mkuu wa shirika hilo, Boniventura Mwalongo, TRAMEPRO ilieleza kuwa marehemu Kardinali Pengo alikuwa mchungaji mwaminifu, kiongozi mwenye hekima na busara, aliyelitumikia Kanisa Katoliki na taifa kwa uaminifu mkubwa, akiacha alama isiyofutika katika mioyo ya wengi.

Shirika hilo limetoa pole kwa Kanisa Katoliki, familia ya marehemu, waumini pamoja na Watanzania wote walioguswa na msiba huo, likisema taifa limepoteza kiongozi wa kiroho aliyekuwa na mchango mkubwa katika malezi ya maadili na mshikamano wa jamii.

TRAMEPRO pia limeungana na waombolezaji wengine kumwombea marehemu apumzike kwa amani ya milele, likisisitiza kuwa maisha yake yanapaswa kuwa funzo kwa jamii kuishi kwa uadilifu, unyenyekevu na utumishi.




SHARE
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment