KAMPENI YA SHAMIRI KUSOMESHA WATOTO 112


SAM_3763
Katikati ni Meneja Mahusiano shirika la The Foundation For Tommorow ,Anton Asukile akifafanua jambo kwa waandishi wa habari jijini Arusha juu ya Kampeni ya SHAMIRI inayolenga kuchangisha milioni 50 kwa ajili ya kusaidia watoto wanaoishi kwenye mazingira hatarishi ,kulia ni Meneja Programu wa masuala ya kijamii na afya Hedwiga Mchaki na kushoto ni Hilda Lema Mfanyakazi wa shirika hilo(Habari Picha na Pamela Mollel wa jamiiblog)
SAM_3747Meneja Programu wa masuala ya kijamii na
afya  wa shirika la The Foundation For Tommorow Hedwiga Mchaki
akifafanua jambo katika kikao na waandishi wa habari jijini Arusha
SAM_3773 Hilda Lema mfanyakazi wa shirika hilo anasisitiza jamii kushiriki katika kampeni hiyo
SAM_3742Taswira
SAM_3803Mwanafunzi wa chuo kikuu Nicemary Phelix aliyewezeshwa na shirika la The Foundation For Tommorow kwa kusomeshwa kwanzia darasa la nne hadi sasa yupo elimu ya juu baada ya kupoteza wazazi wake wote, anaomba watanzania kuonyesha hisia zao katika kusaidia jamii yenye uhitaji na siyo kusubiria wafadhali kutoka nje ya Nchi.
Shirika lisilo la kiserikali la The Foundation for Tommorow limezindua
kampeni ya kuchangia SHAMIRI ya kusaidia elimu ya watoto wanaoishi
kwenye mazingira magumu lengo ni kuchangisha kiasi cha shilingi
milioni 50 zitakazowawezesha kupata elimu bora na kuondokana na
mazingira yanayowakabili.

Meneja Mahusiano wa shirika hilo Anton Asukile alisema hayo jana
akizindua kampeni maalumu ya SHAMIRI inalenga kusaidia ustawi wa
watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi.

“Kampeni hii itawezesha kuinua uchumi wa kaya 40 za watoto wanaoishi
katika mazingira hatarishi kupitia mradi wa WEZESHA KAYA pia
itasaidia upatikanaji wa vifaa muhimu vya kujifunzia kwa watoto
wapatao 112” Alisema Anton.

Asukile ameiomba jamii ya Watanzania kushiriki katika kukabiliana na
changamoto zinazoikabili jamii ili kuwakomboa watoto wanoishi katika
mazingira hatarishi kwa kuchangia kampeni ya SHAMIRI.

Alisema kuwa Watanzania wataweza kuchangia fedha hizo kwa njia ya simu
katika kampeni hiyo imeanza rasmi mwenzi Julai na itahitimishwa
septemba 25 mwaka huu.

Meneja Programu wa masuala ya kijamii na afya Hedwiga Mchaki amesema kuwabaada ya kutoa misaada kwenye familia duni wameona ni vyema wakazipatia mafunzo ya ujasiriamali na mikopo ili waweze kujikwamua na kusomesha watoto wao pasipo kutegemea misaada.
Hedwiga ameitaka jamii ya watanzania kuamka na kusaidia watoto yatima
na wanaotoka kwenye familia masikini badala ya kusubiri mashirika
kuto
SHARE
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment