Magari ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kwa yaliyogharimu zaidi ya Sh.Milioni 42 za matengenezo ikiwa ni sehemu kusaidia ofisi hiyo wafanyakazi kusafiri kutoka sehemu moja kwenda nyingine kutoa huduma kwa wananchi.
Sehemu ya wananchi wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, RC Paul Makonda leo jijini Dar Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akiingia katika moja ya gari ambayo imetengenezwa na umoja wa mafundi gereji bure ikiwa ni sehemu ya mchango wao ufundi katika serikali leo jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza na viongozi wa umoja wa mafundi gereji ambao walikuwa wanamkabidhi magari manne waliyotengeneza bure ikiwa ni sehemu ya mchango wao ufundi katika serikali leo jijini Dar es Salaam.

Magari yaliyotengenezwa bure na mafundi hao
Sehemu ya wananchi wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, RC Paul Makonda leo jijini Dar Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akiendesha moja ya gari ambayo imetengenezwa na umoja wa mafundi gereji bure ikiwa ni sehemu ya mchango wao ufundi katika serikali leo jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akiingia katika moja ya gari ambayo imetengenezwa na umoja wa mafundi gereji bure ikiwa ni sehemu ya mchango wao ufundi katika serikali leo jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akitesti moja ya gari ambayo imetengenezwa na umoja wa mafundi gereji bure ikiwa ni sehemu ya mchango wao ufundi katika serikali leo jijini Dar es Salaam.
---
---
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
UMOJA wa Mafundi wa Gereji wa Wilaya Kinondoni wametengeneza magari ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kwa zaidi ya Sh.Milioni 42 ikiwa ni sehemu kusaidia ofisi hiyo wafanyakazi kusafiri kutoka sehemu moja kwenda nyingine kutoa huduma kwa wananchi.
Akizungumza leo na umoja huo wakati wa kukabidhiwa magari hayo, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema bila ya madereva hao kutokea kuna baadhi ya watumishi walikuwa tayari wanajiandaa kununua magari hayo.
Makonda amesema kuwa kutengeneza magari hayo kuna baadhi ya watu walikuwa wanaombea suala hilo lishindikane lakini mafundi wameonyesha uwezo wao kwa kutengeneza bure ikiwa ni sehemu kuunga mkono juhudi za Rais Dk.John Pombe Magufuli.
Amesema wapo watu wanauwezo lakini wameshindwa kusaidia isipokuwa mafundi wamedhubutu kutengeneza magari ya serikali kwa gharama yao wenyewe.
Makonda amesema kuwa mafundi gereji kwa mara ya kwanza watakuwa wameandika historia ya dunia kujitoa kwa kutengeneza magari serikali bure watumishi wasiweze kutengeneza mazingira ya kukaa ofisini kutokana na kukosa usafiri.
Mkuu wa Mkoa kwa awamu ya kwanza amekabidhiwa magari manne yaliyongenezwa na mafundi gereji yaliyo gharimu zaidi ya sh.milioni 17 na magari mengine yatagharimu za zaidi ya sh.milioni 25 .
Amesema safari ya magari nane kupelekwa tegeta yaliondolewa kwa Break Down na zingine kubebwa na gari kutokana magari hayo hata tairi zake zilikuwa haziwezi kuzunguka.
Aidha amesema mafundi gereji ni watu wanyonge lakini wamekuwa mstari wa mbele hivyo wanahitaji kusaidiwa kwa nguvu zote pale wanapohitaji msaada katika serikali.
Wakati huo huo Umoja wa Mafundi Gereji hao wamemkabidhi madawati 100 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ikiwa kuunga kampeni ya mkuu wa mkoa huyo ya kuchangia madawati.
0 comments:
Post a Comment