IRELAND YAWAKABIDHI SCHOLARSHIP WATANZANIA 14 KUSOMEA SHAHADA YA UZAMILI

 Balozi wa Ireland nchini Tanzania, Bi. Fionnuala Gilsenan, akizungumzia kuhusu ufadhili kwa Watanzania wanaokwenda vyuo mbalimbali vya ndani na nje ya nchi. Sherehe hizo zimefanyika Alhamisi, Agosti 20, 2015 kwenye ofisi za ubalozi huo Masaki jijini Dar es Salaam. (Picha na habari na Daniel Mbega wa www.brotherdanny.com).

Baadhi ya wanufaika wa ufadhili huo wakimsikiliza Balozi wa Ireland (hayuko pichani).
 Baadhi ya wafanyakazi na wageni waalikwa wakimsikiliza Balozi Gilsenan.
 Deogratias Gabriel Rugarabamu, Ofisa Tabibu wa Wilaya ya Kilindi, akipokea cheti cha shukrani baada ya kuhitimu shahada ya uzamili ya Medical Entomology and Clinical Parasitology katika Chuo Kikuu cha Tumaini, KCMC .
Balozi Fionnuala Gilsenan wa Ireland akimpongeza Rubea Mohammed Ali, Mkuu wa Idara katika Wizara ya Kilimo na Maliasili, Zanzibar baada ya kuhitimu shahada ya uzamili katika Chuo Kikuu cha Sokoine katika Elimu ya Kilimo na Ushauri (Agricultural Education and Extension).
David Eliatosha Lekei, Ofisa Kilimo Wilaya ya Hai akipokea cheti cha shukrani kutoka kwa Balozi wa Ireland nchini, Bi.Fionnuala Gilsenan baada ya kuhitimu shahada ya uzamili kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine katika Elimu ya Kilimo na Ushauri (Agricultural Education and Extension).
 Mshereheshaji akisoma majina ya wanufaika.
Stella Zakayo Munisi, Meneja Rasilimali Watu na Utawala wa Shirika la Sikika, akipokea hati ya ufadhili kwenda kusomea shahada ya uzamili kuhusu Organizational Development and Change katika Chuo Kikuu cha Dublin, Ireland. 

Na Daniel Mbega.

SERIKALI ya Ireland kupitia Ubalozi wake nchini Tanzania, leo Agosti 20, 2015 imekabidhi scholarship kwa Watanzania 14 ambao watakwenda kusomea kozi mbalimbali za shahada ya uzamili (masters) ambapo wanne kati yao wakienda kusoma vyuo vikuu nchini Ireland.
Akikabidhi hati hizo za ufadhili wa masomo, Balozi wa Ireland nchini Tanzania, Bi. Fionnuala Gilsenan, alisema utaratibu wa kutoa ufadhili kwa wataalamu mbalimbali ni jambo la msingi kutokana na ukweli kwamba ujuzi watakaoupata unaweza kuliletea taifa maendeleo.

“Ufadhili huu ni sehemu ya Mpango wa Mafunzo wa Kila Mwaka (Fellowship Training Programme), katika sukuma mbele maendeleo ya nchi washirika wetu, tunadhani tunao wajibu wa kusaidia pia kuwaelimisha watalaamu wao,” alisema.

Aliwataja wanufaika wanne waliobahatika kwenda ng’ambo kuwa ni Stella Zakayo Munisi, Meneja Rasilimali Watu na Utawala wa Shirika la Sikika, ambaye anakwenda kusomea shahada ya uzamili (Organizational Development and Change) na Cosmas Joseph Mworia, Ofisa Ushirika na Ofisa Ufuatiliaji na Ukadiriaji katika Kilimo wa Halmashauri ya Wilaya Kondoa anayekwenda kusomea shahada ya uzamili katika Kilimo Endelevu na Maendeleo Vijijini (Sustainable Agriculture and Rural Development). Wawili hao wanakwenda katika Chuo Kikuu cha Dublin.


Flavian Majenga Lihwa, Mratibu Programu ya Elimu wa Shirika la Care Tanzania yeye anakwenda Chuo Kikuu cha Dublin Institute of Technology kuchukua shahada ya uzamili katika Maendeleo Endelevu (Sustainable Development) na Zabron Elias Masatu, Mganga Mkuu wa Wilaya (DMO) ya Misenyi yeye anakwenda Chuo Kikuu cha Taifa cha Ireland Maynooth (NUIM) kuchukua shahada ya uzamili ya Immunolojia na Afya (Immunology and Global Health).

Wanufaika wengine 10 wa mwaka huu, kozi na vyuo wanavyokwenda vikiwa kwenye mabano ni, Siwajibu Ally Selemani Malenge, Kaimu Ofisa Kilimo/Umwagiliaji na Ushirika wa Wilaya ya Kigoma (Chuo Kikuu cha Sokoine – Elimu ya Kilimo na Ushauri ‘Agricultural Education and Extension’); Edita Byangwamu Rutatora Kokwijuka, Ofisa Kilimo Daraja la Kwanza kutoka Wilaya ya Muheza (Chuo Kikuu cha Sokoine – Kilimo); Doreen Elias Mangesho, Mhasibu Mkuu wa CCBRT (Chuo Kikuu cha Dar es Salaam – Utawala wa Fedha); Elinlaa Michael Kivaya, Mchumi wa Kilimo wa Wilaya ya Ngorongoro (Chuo Kikuu cha Sokoine – Kilimo na Uchumi Mtambuka ‘Agriculture and Applied Economics’); na Joshua Julius Musimu, Mkufunzi wa Kilimo Daraja la Pili kutoka Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika (Chuo Kikuu cha Sokoine – Uchumi wa Kilimo ‘Agricultural Economics’).


Wengine ni Fredrick Pius Massawe, Ofisa Kilimo Daraja la Kwanza kutoka Ofisi ya Katibu Tawala Mkoa wa Kilimanjaro (Chuo Kikuu cha Sokoine –Kilimo); Samuel Korinja Olekao, Mratibu wa Kinnapa Development Programme (Chuo Kikuu cha Sokoine – Utunzaji wa Maliasili na Kilimo Endelevu); Eva Emmanuel Mbambale, Ofisa Program wa Sikika (Chuo Kikuu cha Makerere,Uganda – Afya ya Jamii); Iddi Alfani Shekabugi, Mchumi Daraja la Kwanza katika Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika (Chuo Kikuu cha Mzumbe – Uchumi na Fedha kwa Maendeleo); na Felix Lyope Lubuga, Ofisa Utafiti wa Taasisi ya Afya Ifakara (Chuo Kikuu cha Dar es Salaam – Afya ya Jamii).

Awali, Balozi Fionnuala aliwatunuku vyeti wanufaika wengine 10 waliomaliza mwaka 2013 na 2014 katika fani mbalimbali.
SHARE
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment