SIKU YA KIMATAIFA YA VIJANA DUNIANI YAADHIMISHWA KWA RISALA NA BURUDANI


 Vijana kutoka vikundi mbalimbali wakitoa burudani wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya vijana duniani  katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam Agosti 12, 2015
 Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia idadi ya watu duniani (UNFPA) Bibi. Natalia Kanem akizungumza na vijana wakati wa Maadhimisho ya siku ya kimataifa ya vijana duniani leo katika Viwanja vya Mnazi Mmoja. Kushoto ni Mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel
 Kijana ambaye ni mwanachama wa asasi ya vijana chini ya umoja wa mataifa (YUNA) Bw. Hesein Melele akiwasilisha maazimio yaliyofikiwa na vijana wakati wa kongamano lililofanyika Agosti 10 mwaka huu kujadili ujumbe wa siku ya kimataifa ya vijana duniani na kuandaa maazimio yaliyowasilishwa kwa mgeni rasmi leo katika Viwanja vya Mnazi Mmoja walipokua wakiadhimisha siku ya kimataifa ya vijana duniani.
 Naibu Katibu Mkuu kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (kushoto) akiwahutubia vijana walioshiriki maadhimisho ya siku ya kimataifa ya vijana duniani leo katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia idadi ya watu duniani (UNFPA) Bibi. Natalia Kanem.
 Baadhi ya vijana wakifuatilia kwa makini matukio mbalimbali yaliyokua yakiendelea wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya vijana duniani leo katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

 Naibu Katibu Mkuu kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (kushoto) akisikiliza kwa makini maelezo kutoka kwa Afisa Vijana Bi. Amina Sanga (kulia) alipotembelea banda la Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya vijana duniani yaliyoadhimishwa leo katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. Wapili kulia ni Mkurugenzi Maendeleo ya Vijana Bw. James Kajugusi.
 Baadhi ya vijana kutoka shule mbalimbali wakiandamana kuingia katika viwanja vya mnazi mmoja wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya vijana duniani iliyoadhimishwa leo jijini Dar es Salaam na kuhusisha mashirika mbalimbali ya mataifa yanayofanya shughuli za vijana yakiwemo UNFPA, IYF, UNIC, ILO, RESTLESS DEVELOPMENT, YUNA, AMREF, MARIE STOPES, pamoja na PSI.
 Mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (wapili kulia) akipokea maandamano ya vijana (hawapo pichani) wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya vijana duniani iliyoadhimishwa katika Viwanja vya Mnazi Mmoja leo jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi Maendeleo ya Vijana Bw. James Kajugusi na wapili kushoto ni Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia idadi ya watu duniani (UNFPA) Bibi. Natalia Kanem.
SHARE
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment