Mkurugenzi
wa Manispaa ya Kinondoni Mhandisi Mussa Natty akitoa neno la shukrani
baada ya kupokea msaada wa madawati na vifaa vya elimu kwa ajili ya
shule ya msingi Mbuyuni kutoka kampuni ya Aggrey&Clifford kupitia
taasisi ya Hassan Maajar Trust,wengine pichani wa kwanza kulia ni
Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Mbuyuni Dorothy Malecela,katikati ni
Afisa Mtendaji wa Taasisi ya Hassan Maajar Trust Bi.Zena Tenga na
kushoto ni Mkurugenzi wa Mawasiliano na Matangazo wa Aggrey&Clifford
Bw.Oliver Mutere.
Mkurugenzi
wa Manispaa ya Kinondoni Mhandisi Mussa Natty (kushoto) akimfundisha
mtoto kusoma akiwa kwenye moja ya chumba chenye madawati yaliyotolewa
kwa shule ya msingi Mbuyuni na kampuni ya Aggrey&Clifford kupitia
taasisi ya Hassan Maajar Trust, (kulia) ni Mkurugenzi wa Mawasiliano na
Matangazo wa Aggrey&Clifford Bw.Oliver Mutere.
Mkurugenzi
wa Manispaa ya Kinondoni Mhandisi Mussa Natty (kulia) na Mkurugenzi wa
Mawasiliano na Matangazo wa Aggrey&Clifford Bw.Oliver Mutere
(kushoto) wakikata utepe kuashirikia ufunguzi wa moja ya darasa la
shule ya Msingi wa Mbuyuni lililowekewa madawati mapya ambayo yametolewa
kwa shule hiyo na kampuni ya Aggrey&Clifford kupitia taasisi ya
Hassan Maajar Trust.
Walimu
wa shule ya msingi Mbuyuni wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi
wa Manispaa ya Kindondoni na maofisa kutoka kampuni ya
Aggrey&Clifford na Taasisi ya Hassan Majaar Trust muda mfupi baada
ya kumalizika hafla ya kukabidhiwa madawati.
Wanafunzi
wanaosoma katika shule ya awali katika shule ya msingi Mbuyuni wakiwa
katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Manispaa ya Kindondoni na
maofisa kutoka kampuni ya Aggrey&Clifford na Taasisi ya Hassan
Majaar Trust muda mfupi baada ya kumalizika hafla ya kukabidhiwa
madawati.
WATOTO wa
shule ya awali ya Mbuyuni iliyopo wilayani Kinondoni jijini Dar es
Salaam wamenufaika na msaada wa madawati kutoka kwa kampuni ya Matangazo
na Mawasiliano ya Aggrey&Clifford yenye thamani ya shilingi milioni
10.Pia kampuni hiyo imetoa vifaa mbalimbali vya kusomea kwa shule hiyo
ambayo pia inatoa elimu kwa watoto wenye ulemavu wa akili.
Msaada
huo umetolewa kupitia taasisi isiyo ya kiserikali ya Hassan Maajar
Trust,nayo ya jijini Dar es Salaam ambayo imekuwa ikijishughulisha na
kuboresha mazingira ya watoto kusomea kwa kutoa misaada ya madawati na
vifaa vya kusomea mashuleni ikiwemo vitabu na tangu ianzishwe tayari
imetoa misaada kwa shule mbalimbali nchini.
Akiongea
katika hafla ya kukabidhi msaada huo iliyofanyika katika shule ya
msingi Mbuyuni Meneja wa Mawasiliano na matangazo wa
Aggrey&Clifford Bw.Oliver Mutere alisema kuwa msaada huo ni kuunga
mkono jitihada za serikali katika kuboresha sekta ya elimu nchini ambayo
inakabiliwa na changamoto mbalimbali.
“Kampuni
yetu ambayo ina mtamdao katika ukanda wa Afrika Mashariki na ikiwa
imeajiri wataalamu wa Nyanja mbalimbali inajua umuhimu wa elimu bora na
ndio maana tumetoa msaada huu kuwawezesha watoto hawa wasome katika
mazingira mazuri ili waje kuwa wataalamu wazuri katika siku zijazo na
tutaendelea kuunga mkono jitihada za kuboresha elimu nchini”.Alisema.
Afisa
Mtendaji Mkuu wa Taasisi Hassan Maajar Trust ZenaTenga, alisema ana
imani kuwa msaada huu utawanufaisha wanafunzi wengi katika shule ya
Mbuyuni watakaotumia madawati haya “Mazingira bora ya kusomea ni jambo
la muhimu katika kuboresha elimu nchini na huwezi kuongelea elimu bora
wakati watoto wanasoma wakiwa wamekaa sakafuni”.Alisema na kutoa wito
kwa makampuni na taasisi zingine kulivalia njuga tatizo la upungufu wa
madawati mashuleni na kulimaliza kabisa.
Kwa
upande wake Mwalimu Mkuu wa Shule ya Mbuyuni Dorothy Malecela
alishukuru kwa msaada huo ambaye shule yake imepata na alitoa wito kwa
wafadhili wengine kuendelea kujitokeza kusaidia jitihada za serikali
katika kukabiliana na changamoto mbalimbali zilizopo katika ufanikishaji
wa kutoa elimu bora.
0 comments:
Post a Comment