SHULE ZA SEKONDARI NCHINI ZASHAURIWA KUWEKEZA KATIKA MATUMIZI YA NISHATI ENDELEVU YA BIOGESI


 Mtalaam wa masuala ya Biogesi na Majiko Sanifu wa Taasisi ya kuendeleza Nishati Asilia na Uhifadhi wa Mazingira Tanzania ( TaTEDO) Bw.Stephen Boniface akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari kuhusu ujenzi wa mtambo wenye uwezo wa kuzalisha gesi yenye mita za ujazo 200 walioujenga katika shule  ya Sekondari Manzese iliyoko wilayani Kinondoni jijini Dar es Salaam jana. Kulia kwake ni Mkuu wa Shule ya Sekondari Manzese Bw.Linus Mwakasege.
 Meneja Uhusiano wa Jamii wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es salaam (DAWASA) Bi.Neli Msuya akielezea ushiriki wa DAWASA katika kufanikisha ujenzi wa Mradi wa Biogesi katika shule ya Sekondari Manzese ya jijini Dar es salaam mara baada ya kutembelea mradi huo jana jijini Dar es salaam.
 Mkuu wa Shule ya Sekondari Manzese Bw.Linus Mwakasege akitoa ufafanusi kwa waandishi wa habari kuhusu manufaa ya mradi wa nishati endelevu ya Biogesi utakavyowanufaisha wanafunzi wa shule hiyo.
 Mtaalam wa Nishati Endelevu na mabadiko ya Tabia nchi Bw. Shima Sango kutoka Taasisi ya Uendelezaji wa Nishati asilia na Uhifadhi wa Mazingira (TaTEDO) Akiwasha moja ya jiko la gesi liliojengwa katika shule ya Sekondari Manzese.
Picha na Aron Msigwa - MAELEZO.
---
SHULE za Sekondari kote nchini zimeshauriwa kuwekeza katika matumizi ya Nishati endelevu ya Biogesi na majiko sanifu ili kulinda na kuhifadhi mazingira.

Ushauri huo umetolewa na Meneja Uhusiano wa Jamii wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es salaam  (DAWASA) Bi.Neli Msuya mara baada ya kutembelea ujenzi wa Mradi wa kuzalisha Nishati endelevu ya Biogesi katika Shule ya Sekondari Manzese wilayani Kinondoni, jijini Dar.
SHARE
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment