Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kampala International cha jijini Dar es Salaam, Rais mstaafu wa Tanzania Mh.Ali Hassan Mwinyi akiongozana na wahadhiri wa Chuo Kikuu hicho wakielekea kwenye uwanja wa hafla ya mahafali yaliyofanyika chuoni hapo eneo la Gongo la Mboto jana.
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kampala International cha jijini Dar es Salaam, Rais mstaafu wa Tanzania Mh.Ali Hassan Mwinyi (watatu kutoka kulia) na viongozi wa chuo hicho wakiwa wamesimama wakati unaimbwa wimbo wa Taifa kabla ya kuanza hafla ya mahafali ya 3 yaliyofanyika chuoni hapo eneo la Gongo la Mboto jana jana ambapo wahitimu walitunukiwa shahada,stashahada na vyeti katika fani mbalimbali.
Sehemu wa wanafunzi waliohitimu chuoni hapo jana.
Makamu Mkuu wa Chuo cha Kampala Internatinal cha Dar es Salaam Profesa Mohamed Ndaula akitoa hotuba wakati wa mahafali 3 yaliyofanyika chuoni hapo eneo la Gongo la Mboto jana jana ambapo wahitimu walitunukiwa shahada,stashahada na vyeti katika fani mbalimbali.
---
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kampala International cha jijini Dar es Salaam,Rais Mstaafu wa Tanzania Mheshimiwa Ali Hasani Mwinyi amewataka watanzania kuchangamkia fursa za masomo ya taaluma mbalimbali nanayotolewa na Chuo Kikuu cha Kampala kilichopo eneo la Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam.
---
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kampala International cha jijini Dar es Salaam,Rais Mstaafu wa Tanzania Mheshimiwa Ali Hasani Mwinyi amewataka watanzania kuchangamkia fursa za masomo ya taaluma mbalimbali nanayotolewa na Chuo Kikuu cha Kampala kilichopo eneo la Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam.
Akiongea
wakati wa mahafali ya tatu ya chuo hicho kwa upande wa Tanzania jana
ambapo wahitimu walitunikiwa shahada ,stashahada na vyeti vya kufuzu
fani mbalimbali alisema chuo hicho kinatoa elimu bora kwenye fani
mbalimbali na kuwataka watanzania kuchangamkia fursa za kujiendeleza ili
wapate maarifa ya kuwawezesha kupambana katika soko la ajira ikiwemo
kupata maarifa ya kuwawezesha kujiajiri kutokana na elimu watakayokuwa
wameipata.
Alipongeza
wawekezaji kwenye sekta ya elimu na kuiomba serikali kushirikiana nao
li nchi iweze kupata wataalamu wa kutosha “Napongeza kwa uwekezaji huu
na tunaomba serikali izidi kuunga mkono wawekezaji katika sekta ya elimu
ili Taifa liweze kupata wataalamu wa kutosha.
Naye
Makamu Mkuu wa Chuo hicho Profesa Mohamed Ndaula alisema kuwa chuo
kimejipanga kuendelea kutoa elimu bora kuanzia kwenye miundombinu na
walimu waliobobea katika fani mbalimbali na uzoefu mkubwa wa kufundisha
vyuo vikuu sehemu mbalimbali duniani.
Pia
alisema kuwa Chuo hicho kimefanikiwa kupata leseni ya kujiendesha
nchini badala ya kuwa Chuo Kikuu kishiriki cha Chuo Kikuu Cha Kampala
kilichopo nchini Uganda.
0 comments:
Post a Comment