MAANDALIZI YA JUBILEI YA MIAKA 50 YA SHULE YA SEKONDARI YA WASICHANA RUGAMBWA

Jumuiya ya wanarugambwa (Rugambwa Girls Foundation) wanayo furaha kukualika kwenye mkutano wa pamoja utakaofanyika tarehe 23 Januari, 2016 kuanzia saa 7 mchana, Leaders Club, Dar es Salaam.

Ukiwa kama mdau wa Rugambwa Sekondari: mwanafunzi, mwalimu, mtumishi wa aina yoyote aliyewahi kupita Rugambwa Sekondari pamoja wanafunzi wote waliosoma shule rafiki za Rugambwa (Ihungo, Kahororo, Bukoba Sekondari, Nyakato, Ntugamo Seminari, n.k. tunakualika kushiriki.
Lengo ni kukutana kubadilishana mawazo na kupeana mikakati jinsi ya kupata fedha kwa ajili ya kufanikisha jubilee ya miaka 50 ya Rugambwa Sekondari itakayofanyika, Machi 2016 pamoja na ukarabati na uboreshaji wa shule hiyo.
Atakayesikia au kusoma tangazo hili amfahamishe na mwingine.
Kwa maelezo zaidi wasiliana na:
Rugambwa Girls Foundation

SHARE
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment