Dk.
Kitua kutoka SACIDS akizungumza jambo wakati wa mkutano wa Wataalamu wa
Afya kutoka vyuo mbalimbali hapa nchi ili kujadili nikwa jinsi gani
wanaweza kushirikiana katika kufanya kazi bila kuangalia kuegemea upande
wowote wa Afya.

Profesa
Mamuya kutoka MUHAS akiwasilisha mada kwenye mkutano uliowashirikisha
wataalamu mbalimbali wa afya ya mifugo, binadamu pamoja na afya ya
mazigira uliofanyika Bagamoyo.






---
Taasisi
za SACIDS na OHCEA wameandaa mkutano uliowakutanisha wataalamu
mbalimbali wenye ujuzi tofauti wa Afya hasa Afya ya Mifugo, Afya ya
Binadamu pamoja na Afya ya Mazingira kutoka kwenye vyuo mbalimbali vya
hapa Tanzania.
Mkutano
huo ulikuwa na lengo la kuweza kuangalia ni kwa namna gani wanaweza
kufanya kazi kwa pamoja bila kubagua upande wowote ili kutatua tatizo
lililokuwepo kwa miaka mingi hapa nchini Tanzania hasa pale yanapotokea
magonjwa yanayowapata mifugo pamoja na binadamu.
Mgeni
rasmi aliyefika katika mkutano huo alikuwa Dk. Deo Mtasiwa ambaye ni
Naibu Katibu Mkuu wa Afya TAMISEMI ambaye alisema kuwa serikali iko
pamoja na wataalamu wa Afya ya Mifugo, Afya ya Binadamu pamoja na Afya
ya Mimea.
Pia
amesema mpango ulioandaliwa na wataalamu hao wa afya wa kufanya kazi
kwa pamoja utachukuliwa na serikali ili kuangalia ni kwa namna gani
wanaweza kuutumia ili ikitokea ugonjwa kwa mifugo kwenda kwa binadamu
iwe ni rahisi kutatua tatizo hilo.
"Magonjwa
ya kuambukia yanayotoka kwa wanyama kwenda kwa binadamu yanaleta
changamoto kubwa sana lakini kwa sababu umekuwepo mpango wa Afya mmoja
basi utatusaidia na pia tutawatumia wataalamu bila kuangalia yuko kundi
gani," alisema Naibu Katibu Mkuu
Pia
alisistiza kuwa umoja wao ndio mafanikio yao kwani wasipoungana na
kufanya kazi kwa pamoja itakuwa ni vigumu kufikia yale malengo
waliyojiwekea. "Napenda kuona mnatoa elimu katika jamii kuhusu magonjwa
ya kuambukizwa ambayo yanatoka kwa wanyama kwenda kwa binadamu ili
kuweza kunusuru maisha ya wananchi walio wengi.
Pia
alisema serikali iko tayari kuwasaidia kwa pale watakapohitaji msaada
wao kwa sababu afya ni kitu cha msingi kwa wanyama pamoja na binadamu na
kuongeza atashirikiana bega kwa bega na wizara kama vile Wizara ya
Elimu na Mafunzo ya Ufundi pamoja na Wizara ya Kilimo na Ufugaji ili
kuweza kufikisha kile walichomtuma kama mtendaji wa serikali.
Pia
ameshukuru taasisi zilizofanikisha mkutano huo ambazo ni OHCEA na
SACIDS zimetengeneza mipango mizuri kwa wataalamu wa afya na kuwaleta
karibu kwa ajili ya kushirikiana.
Akizungumza
Profesa Robson Mdogera ambaye ni mhadhiri na mtafiti mtoa huduma katika
Chuo Kikuu cha Sokoine amesema mkutano huu umekuja wakati muhafaka
kwani kumekuwepo tatizo kubwa la kutoshirikiana katika hali zote.
“Huu
mpango waliokuja nao wa Afya moja unaweza kuleta mafanikio makubwa
maana kuna viwatilifu vinavyowekwa kwenye mifugo au mazao ili kukinga
magonjwa hivyo kunapelekea viwatilifu hivyo kuliwa na binadamu bila
kujua na kupeleka adhari kubwa katika mwili wa binadamu. Hivyo
kunahitaji kuwa na ushirikiano katika nyanja zote za afya ili kuweza
kutatua tatizo pale tu linapotokea,” alisema Prof. Mdogera.
0 comments:
Post a Comment