Mwanafunzi
wa darasa la sita kutoka shule ya msingi kibangile Radia Hamis
akishukuru kwa msaada wa madawati kwa niaba ya wanafunzi wa shule hiyo
kwa Mkurugenzi wa Tigo kanda ya pwani Goodluck Charles katika hafla ya
kukabidhi madawati 400 kwa shula 10 za wilaya ya Morogoro vijijini.
Februari
11 2016 Morogoro: Kampuni ya Tigo Tanzania imetoa msaada wa madawati
400 yenye thamani ya shilingi milioni 60 kwenye shule 10 za msingi
katika mkoa wa Morogoro ikiwa ni mchango wa kampuni hiyo katika
kuisaidia serikali kukabiliana na upungufu wa madawati katika shule za
msingi nchini.
Akizungumza
katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika katika Shule ya Msingi
Kibangile iliyopo Kitemu katika kata ya Matambo, Morogoro Kusini,
Mkurugenzi wa Tigo wa Kanda ya Pwani Goodluck Charles mchango huo ni
sehemu ya utekelzaji dhamira ya kampuni hiyo ya kuunga mkono shughuli
mbalimbali za maendeleo nchini.
“Mchango
huu ni sehemu ya jitihada mbalimbali zinazofanywa na Tigo katika
kusaidia utekelezaji wa miradi yenye tija kubwa kwa jamii. Tunaamini
kwamba kupitia msaada huu, Tigo inatoa mchango wake katika kujenga
viongozi wa baadaye wa taifa hili na wanataluuma mbalimbali wakiwamo
madaktari, wahandisi na wengineo, "alisema Charles.
Charles
alisema mwaka jana Tigo ilikabidhi msaada kama huo wa madawati katika
shule za msingi katika mikoa ya Shinyanga, Mbeya na Iringa na kuongeza
kwamba kampuni hiyo itaendelea kutoa madawati zaidi sehemu mbalimbali
nchini siku za zijazo.
Makabidhiano
yalihudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dr Rajabu Rutengwe ambaye
alisema madawati hayo 400 yataboresha mazingira ya kujifunzia kwa watoto
katika Mkoa wa Mporogoro na kutoa wito kwa wadahu wengine kuunga mkono
zoezi hilo.
“Tunapenda
kutoa shukrani zetu za dhati kwa kampuni ya Tigo kwa kuwa mdau muhimu
kwetu katika jitihada zinazoendelea za kujaribu kupunguza tatizo la
ukosefu wa madawati ya kutosha katika shule za msingi za mkoa wetu wa
Morogoro. Ni Dhahiri kwamba msaada huu wa madawati 400 yatawawezesha
mamia ya wanafunzi wetu kupata sehemu za kukaa na hivyo kujipatia elimu
zao katika mazingira bora Zaidi,” alisema Dr Rutengwe.
0 comments:
Post a Comment