DUA YA KUMUOMBEA MWANA WA CHUONI MKUBWA NCHINI TANZANIA NA ULIMWENGUNI KWA UJUMLA KUFANYIKA KTK JIJI LA LONDON NCHINI UINGEREZA


Kufuatia kifo cha mwana wa chuoni mkubwa nchini Tanzania na ulimwenguni kwa ujumla Sheikh Muhammad ibnu Abii Bakaril Burhaan ambae alikuwa ni mkuu wa chuo cha Shamsul Maarif kilichopo mkoani Tanga, imeonekana ni busara kufanya dua ya kumuomba Allah amfanyie wepesi ktk safari yake.

Fikra imekuja sio tuu kwa kukiri mchango wake mkubwa kwa wa- Islam na u- Islam lakin kwa wanadamu kwa ujumla. Dua imepangwa kufanyika Jumamosi ya tarehe 19/03/2016 saa nane mchana maeneo ya Barking, East London ukumbi utatajwa baadae.

Masheikh wengi na wadau mbali mbali wanategemea kuhudhuria na tunawaomba wote watakao jaaliwa tushirikiane ili kufanikisha jambo hili tukufu.

Kwa mawasiliano zaidi na yote yanayo husu shughuli nzima wasiliana kwa namba zifuatazo: 07986142485 au 07904962787 au 07453530218. Mahudhurio yako ndio mafanikio ya shughuli hii. Mnakaribishwa.
SHARE
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment