TRA WAFUNGA MRADI WA MAFUNZO KATI YA TANZANIA NA JICA

MAMLAKA YA MAPATO TANZANIA(TRA) yafunga mradi wa miaka minne kati ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania na Shirika la  maendeleo la Japani (JICA) la Serikali ya Japani  mara baada ya  mradi huo kumaliza muda wake.

 Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurgenzi wa Rasilimali watu Mamlaka ya Matapo Tanzania(TRA), Victor Kimaro alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, amesema kuwa  Mradi huo umewanoa wafanyakazi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania pamoja na wanafunzi 608 na umeghalimu kiasi cha dola za kimarekani milioni3.5.

Pia amesema mradi huo wa Shirika la  Maendeleo la Japani (JICA) wa Serikali ya Japani umesaidia kuboresha mafunzo kwa  wafanyakazi na wafanyakazi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA).

Mwisho wa Mradi huo ni mwamzo wa kuanzisha mradi mwingine wa mafunzo na kuboresha ukusanyaji wa mapato hapa nchini.

Mradi uliokuwa unaitwa  'PROJECT FOR ENHANCEMENT OF TAXATION TRAINING IN TANZANIA.'
 Kaimu Mkurgenzi wa Rasilimali watu Mamlaka ya Matapo Tanzania(TRA), Victor Kimaro akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusina na kufunga mkataba wa miaka minne kati ya Tanzania na Japani mkataba ambao ulikua unatoa mafunzo ya kukusanya Kodi hapa nchini kwa wanafunzi wa chuo cha kodi (TRA) pamoja na wafanyakazi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA). Kushoto ni  Msimamizi wa Mradi wa Shirika la  maendeleo la Japani (JICA), Toshio Nagase.
Msimamizi wa Mradi wa Shirika la  maendeleo la Japani (JICA), Toshio Nagase akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo. kulia ni Kaimu Mkurgenzi wa Rasilimali watu Mamlaka ya Matapo Tanzania(TRA), Victor Kimaro.
 Mkuu wa Chuo cha Kodi (TRA), Isaya Jairo(Kushoto) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa kufunga mkataba wa mradi wa miaka minne ambao ulikuwa unatoa mafunzo kwa wafanyakazi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) na wanafunzi wa chuo cha kodi. Kulia ni Kaimu Mkurgenzi wa Rasilimali watu Mamlaka ya Matapo Tanzania(TRA), Victor Kimaro. Picha na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.
SHARE
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment