Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Halima Dendego(katikati) akikata utepe katika makabidhiano ya kompyuta ishirini zenye thamani ya 33m/- zikiwa na huduma ya intaneti ya bure iliyo gharimu 22m/- katika Shule ya Sekondari Sino,mkoani Mtwara, kushoto ni Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Pwana Goodluck Charles, na kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Fatuma.
Wanafunzi wakishuhudia makabidhiano hayo |
Kampuni inayoongoza kwa maisha ya kidijitali ya Tigo Tanzania leo imetoa kompyuta 20 zenye thamani ya shilingi milioni 33 zikiwa na huduma ya bure ya intaneti iliyogharimu 22m/- kwa shule tatu za sekondari mkoani Mtwara.
Msaada huo uko katika mkondo wa malengo ya kampuni ya kuleta
mabadiliko ya kidijitali katika sekta ya elimu nchini.
Akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano yaliyofanyika Shule ya Sekondari Sino mkoani Mtwara Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Pwani, Goodluck Charles alisema, “Msaada huu kwa shule hizi tatu ni sehemu ya mkakati wa kampuni wa kuleta mageuzi katika mtindo wa maisha ya kidijitali.
Msaada huu wa leo umekuja baada ya kukabidhi kompyuta 10 kwa Shule ya Msingi Chuda mkoani Tanga na kompyuta 25 zilizounganishwa na intaneti kwa Hospitali ya Rufaa ya Sekou Toure mkoani Mwanza mwaka jana.
“Msaada kwa shule ya Sekondari ya Masasi, Tandahimba na Sino ni kielelezo cha kweli cha uwekezaji wa Tigo katika miradi tofauti yenye mchango kijamii kupitia mkakati wetu wa kuwekeza kijamii unaowezesha jamii kupokea zana za kisasa za Teknolojia ya Habari na Mawasiliano katikanyanja zote za kijamii ikiwemo sekta ya elimu,” alisema Charles.
Tukio hilo ambalo lilihudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Halima Dendego ambaye alizitaka sekta binafsi kuisaidianserikali katika mikakati yake katika kuboresha mazingira ya kujifunzia katika
shule zilizopo nchini.
Dendego alisema, “Naipongeza Tigo kwa ukarimu wao wa kuzisaidia shule hizi natoa wito kwa watu binafsi kampuni za biashara na wadau wengine kujitokeza katika kuunga mkono juhudi za kuboresha
sekta ya elimu.”
Akipokea msaada huo kwa niaba ya wakuu wenzake wa shule za sekondari, Mkuu wa Shule ya Sekondari Sino Riyadh Kadhi alisema kwamba kompyuta hizo zitawawezesha wanafunzi kuwa na uelewa wa kiteknolojia na kuwawezesha kuipata teknolojia ya habari mapema katika elimu yao.
“Tunafurahi kwa hatua hii ya Tigo; tuna matumaini kwamba kompyuta hizi zitawaweka wanafunzi wetu katika ngazi moja na wenzao katika mashule mengine yaliyo maeneo ya mjini na duniani kwa
ujumla,” alisema Kadhi.
0 comments:
Post a Comment