Mkuu wa Idara ya Uhandisi Mazingira (Environmental Engineering) Dr. Fredrick Salukele akiwaelezea wanafunzi matumizi ya vifaa mbalimbali vitumikavyo kwenye shughuli za ufundishaji, utafiti na utoaji ushauri wa kitaalam, mfano wa vifaa hivyo ni Gaschromatograph kinachoonekana kwenye picha.
Wanafunzi wa Shule ya Mtakatifu Maximilian walipotemblea Maabara ya Sayansi ya Mazingira na Tekinolojia ya Chuo Kikuu Ardhi. Maabara hiyo hutumika kwa ajili ya shughuli za Ufundishaji, Utafiti na Uhauri wa kitaalamu katika fani ya Sayansi ya Mazingira.
Wanafunzi wakiangalia kwa makini baadhi ya kazi za ubunifu majengo zilizo fanywa na wanafunzi wa Skuli ya Ubunifu Majengo wa Chuo Kikuu Ardhi. Kubuni aina mbalimbali za majengo ni moja kati ya mahitaji kwenye mtaala wa kufundishia program ya Usanifu Majengo ya Chuo Kikuu Ardhi
Mtaalam kutoka Skuli ya Sayansi ya Jiomatiki wa Chuo Kikuu Ardhi Bw. Pius Lugomela (mwenye shati la bluu), akitoa malezo kuhusu vifaa mbalimbali vya upimaji ramani vilivyoko kwenye maabara ya Skuli iyo.Vifaa kwenye maabara hiyo pia hutumika kwa ajili ya shuguli za ufundishaji, utafiti na ushauri wa kitaalamu kwenye maenneo ya upimaji ardhi na ramani.
Na. Hadija Maulid - Chuo Kikuu Ardhi.
Chuo Kikuu Ardhi kimetoa wito kwa wanafunzi wanaosoma darasa la saba kote nchini kufanya bidii katika masomo ya Sayansi na Hisabati ili waweze kujenga msingi imara na kuandaa mazingira ya kujiunga na fani za Sayansi katika elimu ya Sekondari na vyuo vikuu.
Wito huo huo umetolewa leo jijini Dar es salaam na baadhi ya wataalamu wa Chuo hicho mara baada ya kuwapokea wanafuzi 84 wa Shule ya Msingi ya Mtakatifu Maximilian waliotembelea maeneo mbalimbali ya chuo hicho kwa lengo la kujifunza majukumu ya chuo hicho na elimu inayotolewa.
Wakiwa chuoni hapo wanafunzi hao wamepata fursa ya kuitembelea Skuli ya Sayansi ya Mazingira na Teknolojia (Environmental Science and Technology) Skuli ya Ubunifu Majengo (School of Architecture and Design) na Skuli ya Sayansi ya Jiomatiki na Tekinolojia (School of Geospatial Sciences and Technology).
Aidha, Wanafunzi hao walipata fursa ya kuuliza maswali mbali mbali kwa wataalamu.
Ziara hiyo imelenga kuwahamasisha wanafunzi kufanya vizuri katika masomo ya Sayansi ili waweze kupata alama za juu zitakazowawezesha kuendelea na masomo ya kidato cha tano na sita na kisha kujiunga na Chuo kikuu Ardhi ili baadaye wawe wataalamu katika fani mbalimbali za Ardhi na Mazingira.
0 comments:
Post a Comment