Mkurugenzi wa Light for the World Joseph Banzi Akizungumza na waandishi wa habari katika Mkutano wa Wadau wa elimu jumuishi uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Shirikisho la Watu wenye Ulemavu (Shivyawata) Ernest Kimaya akizungumza kuhusiana na elimu jumuishi katika mkutano wa wadau ulifanyika jijini Dar es Salaam.
Mratibu la Light For the World Belgium Koen Lein akizungumza kuhusiana elimu jumuishi katika mkutano uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Na Chalila Kibuda, Michuzi TV
TAASISI ya Light for the World imesema kuwa asilimia 70 ya watoto wenye ulemavu wa macho waliosaidiwa kupatiwa vifaa vya kusomea na kupewa kipaumbele shuleni, walifaulu elimu ya msingi na kijiunga na sekondari na sasa wanatarajia kuwasaidia elimu ya sekondari.
Watoto wenye ulemavu wa macho waliosaidiwa na kufaulu elimu ya msingi na kwenda sekondari huko wasiposaidiwa usaidizi huo wa awali utakuwa umewakomboa.
Hayo yalielezwa na Mkurugenzi Shirika la Light For The World, Joseph Banzi, wakati akizungumza na waandishi wa habari, katika mkutano wa wadau mbalimbali wa kujadili namna watu wenye ulemavu wanapata fursa ya kuendelea na masomo bila ya kujali changamoto na ndioa maana serikali imeweka miongozo na sera kuhakikisha hakuna mtoto atakayeachwa nyuma.
Amsema taasisi hiyo yenye miaka mitano tangu kuanzishwa kwake, iliwasaidia watoto wenye ulemavu kupata elimu na asilimia 30 pekee kati ya idadi yote ndio walioshindwa kuendelea na masomo ya sekondari hivyo jitihada zaidi inafanyika katika kuhakikisha wanafunzi wenye ulemavu wote wanapata elimu.
Taasisi hiyo kwa sasa ina jumla ya watoto wenye ulemavu wa macho 311, kutoka katika mikoa ya Mororogo na Dodoma.
Amesema lengo la mkutano huo ni kubadilisha uzoefu kulingana na changamoto za watoto wenye ulemavu na namna kuwasaidia watoto hao.Alisema yapo mashirika mbalimbali yanayofanya kazi tofauti hivyo wamekutana kuona namna ya kushirikiana katika kuwasaidia watoto hao.
Aidha, alitaja aina ya changamoto zinazowakabili watoto wenye ulemavu ni kukosa matibabu na kukosa vifaa vya kuwasaidia kupata elimu.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Watu wenye Ulemavu (SHIVYAWATA), Ernest Kimaya, alisema wanaangalia njia bora zaidi ya kupata elimu jumuishi.
Amesema tafiti zinaonyesha kuwa, changamoto bado zipo zinafanya watoto wenye ulemavu kushindwa kupata elimu.
Changamoto ni ukosefu wa walimu wenye taaluma ya ulemavu na vifaa vya kufundishia na kwamba kuna sera za kuwajumuisha wanafunzi wote kupata elimu hata walio na changamoto za ulemavu bila ya ubaguzi.
Aidha, alisema jamii ina nafasi kubwa ya kuhakikisha inawatambua watoto wenye changamoto ya ulemavu.
“Mara nyingi wanaachwa nyumbani na wengine wanafungiwa ndani. Jamii inaweza kuwasaidia kwa kuwapazia sauti na pia inaweza inaweza kuchangia kwenye miundomboni kupitia kamati za shule,” alisema Kimaya.
Mkutano wa wadau wa juu ya elimu jumuishi.
0 comments:
Post a Comment