Matengenezo Kinyerezi Mbioni Kukamilika

Na Mwandishi Wetu – Dar es Salaam.

Wakazi wa Kata ya Kinyerezi, Jijini Dar es Salaam, wametangaziwa kurejea kwa huduma ya majisafi mapema leo, Agosti 4, 2025, kufuatia kukamilika kwa matengenezo ya bomba la usambazaji maji lililoathiri maeneo mengi ya kata hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mhandisi wa Usambazaji Maji kutoka Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA), Antony Budaga, amesema matengenezo hayo yamehusisha ubadilishaji wa kipande cha bomba la inchi 12 kwa umbali wa takribani mita 310, kwa lengo la kuboresha huduma ya maji kwa wakazi wa Kinyerezi.

“Kama Mamlaka tunaomba radhi kwa wananchi wote walioathirika na marekebisho haya ambayo yamesababisha kukosekana kwa huduma. Kazi hii imefanyika usiku na mchana ili kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma. Tunatarajia kukamilisha kazi hii jioni ya leo na huduma kuanza kurejea kwa kasi katika maeneo mbalimbali,” alisema Mhandisi Budaga.

Maeneo yanayotarajiwa kurejea kwa huduma ni pamoja na Sabasaba, Stakishari, Mongo la Ndege Shule ya Msingi, Mpera, Mwembeni, Mnembwe kwa Balozi Vick, Zimbili A (Darajani), St. Rosalia, Zimbili kwa Balozi, Serikali ya Mtaa Zimbili, Kwa Diwani Leah, Mwaipaya, Mnembwe, Garage ya Wachina, Mnara wa Voda, Kwa Smart, Kwa Makadali, NSSF Kota, Mbuyuni, Saloon Mafuta ya Taa, Ngekili, Msikitini, Shule ya Msingi Kinyerezi, Kanga Chini, Mtaa wa Uzinguni, Machinjio ya Nguruwe, Kwa Kipofo, Kanisa la Wasabato Kanga Chini, Kwa Angles, Mtaa wa Kwa Tozi, Maduka Saba, New Vibe, Michael Mausa, BL Park, Kinyerezi Park, Flamingo, Njombe Road, Zimbili Msikitini wa Njano, Kwa Simba Chawene na Kwa Msemwa.

DAWASA imewahakikishia wakazi wa maeneo hayo kuwa huduma itaendelea kuimarika kadri kazi ya uunganishaji wa bomba jipya inavyokamilika.

SHARE
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment