WATEJA WA BENKI YA CRDB WAFURAHIA HUDUMA WAKIJIZOLEA ZAWADI

Kampeni ya TUSHAVUKA HUKO ya Benki ya CRDB inaendelea kuvunja rekodi baada ya wateja kutoa ushuhuda kuhusu maboresho makubwa ya mfumo na huduma za benki hiyo, huku wakijipatia zawadi mbalimbali ikiwemo fedha taslimu hadi Shilingi Milioni Moja, Bima ya Afya kwa mwaka mzima, na Bima ya KAVA inayotoa mkono wa pole pale mteja anapopata ulemavu wa kudumu, kufariki au kufiwa na mwenza.

Stephen Adil, Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi, alisema maboresho yaliyofanywa kwenye mfumo wa Benki ya CRDB yameongeza kasi, usalama na ufanisi wa huduma kwa kiwango ambacho hakijawahi kushuhudiwa.
Adili amesema maboresho haya yemeongeza ubora katika huduma zote kuanzia matawini, CRDB Wakala, ATM, pamoja na kwenye majukwaa ya kidijitali ikiwamo SimBanking, Internet Banking, pamoja na majukwaa ya malipo mtandaoni kupitia Lipa Hapa, POS na TemboCard, ambapo sasa huduma zinapatikana kwa usalama wa hali ya juu, na kwa kasi zaidi.”

Kwa upande wa huduma za SimBanking, wateja wengi wamesema huduma zimekuwa na kasi zaidi kuliko mwanzo. Bw. Patrick Msuya, mfanyabiashara wa Kariakoo, anasema SimBanking ndiyo sasa imekuwa “msaidizi wake wa kila siku.”

“Nikituma pesa kwa msambazaji, malipo yanafanyika kwa haraka zaidi. Malipo ya umeme, maji na hata kodi za TRA sasa malipo ni sekunde tu. Nilisikia Benki ya CRDB imeboresha mfumo, lakini sikujua ni maboresho yenye ubora wa kiwango hiki. Tunawapongeza na kuwashukuru sana.”

“Kitu cha kufurahisha zaidi, kila muamala ninaoufanya unanipa nafasi ya kushinda Milioni Moja. Hii imekuwa motisha ya kipekee,” alisema.
Takwimu za benki zinaonesha matumizi ya majukwaa ya kidijitali ya kutolea huduma ikiwamo SimBanking yamepanda kwa kasi tangu kuanza kwa kampeni ya TUSHAVUKA HUKO baada ya kukamilika kwa maboresho ya mfumo, huku malalamiko ya ucheleweshaji au mfumo kukwama yakipungua kwa zaidi ya asilimia 95.

Kwa upande mwengine, huduma za TemboCard nazo zimeendelea kuvutia wateja hasa baada ya Benki ya CRDB kutangaza msimu wa zawadi kwa wanaofanya manunuzi kwenye maduka, migahawa, hoteli, vituo vya mafuta, na sehemu mbalimbali za malipo nchini.

Wikiendi hii, Benki imetua katika maduka ya Shoppers Supermarkets nchini ikiwa na kauli mbiu “Beba TemboCard yako kisha chanja tukuzawadie.”

Bi Stella Nyakato, mkazi wa Mbezi Beach, alikuwa miongoni mwa waliojitokeza kufanya manunuzi. “Nilichanja TemboCard yangu tu baada ya kulipa, Afisa Mauzo wa Benki ya CRDB aliyekuwepo pale akaniambia ‘Hongera, umepata zawadi.’ Sikuamini nilihisi kama benki inanijali binafsi,” alisema kwa shangwe.

“Nimekuwa mteja wa Benki ya CRDB miaka mingi, lakini huu mwaka naona mabadiliko ambayo sijawahi kuyaona. Huduma ni za kasi sana, hata POS hazikati kama zamani.”

Maboresho ya mfumo yaliyofanyika pia yameongeza uwezo wa CRDB Wakala kuhudumia wateja kwa haraka, kupitia utoaji wa fedha, kuweka fedha, malipo ya ankara na huduma nyingine.

“Kasi ya huduma imeongezeka maradufu. Mteja akija, hata kama foleni ipo, ndani ya sekunde chache anahudumiwa. Mfumo haukatiki, na hii imetupa heshima kubwa katika jamii. Wateja wanafurahia zaidi kwa sababu kila muamala pia unawaingiza kwenye droo za zawadi,” anaeleza Bw. Ramadhani Salim, wakala wa CRDB eneo la Kigogo.

Benki ya CRDB imesema promosheni hii itaendelea kwenye maeneo mbalimbali, ikiwawezesha wateja kufurahia ununuzi na kupata zawadi papo hapo.

“Urahisi zaidi, kasi zaidi na ubora zaidi si kauli tu ni uhalisia ambao wateja wetu wanaouona na kuuishi kila siku,” alisema Adili. 

“Kampeni ya TUSHAVUKA HUKO imedhihirisha kuwa huduma bora zinapounganishwa na zawadi, mteja anajisikia kuthaminiwa na kuwa sehemu ya safari ya benki.”
SHARE
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment