Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso (wa tatu kulia),
akizungumza kabla ya kukabidhi Darasa la Chekechea lililokarabatiwa
kwa udhamini wa Wafanyakazi wa Airtel, kama sehemu ya huduma kwa
jamii, katika Shule ya Msingi Ushindi iliyopo Mikocheni ‘B’, jijini
Dar es Salaam jana. Kutoka (kulia) ni Mwenyekiti wa Shule hiyo,
Jumanne Konara na Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Elias Katunzi, Meneja wa
Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (kushoto) na baadhi ya
wafanyakazi wa kampuni hiyo.
Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso (wa tatu kulia),
akimkabidhi Mtendaji wa Serikali ya Mtaa wa Mikocheni ‘B’, Suleiman
Sagong’o, Darasa la Chekechea lililokarabatiwa kwa udhamini wa
Wafanyakazi wa Airtel, kama sehemu ya huduma kwa jamii, katika Shule
ya Msingi Ushindi iliyopo Mikocheni ‘B’, jijini Dar es Salaam jana.
Kutoka (kulia) ni Mwenyekiti wa Shule hiyo, Jumanne Konara na Mwalimu
Mkuu wa shule hiyo, Elias Katunzi, Meneja wa Huduma kwa Jamii wa
Airtel, Hawa Bayumi (kushoto) na baadhi ya wafanyakazi wa kampuni
hiyo.
Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso (kulia), akifungua
mlango wa Darasa la Chekechea lililokarabatiwa kwa udhamini wa
Wafanyakazi wa Airtel, kama sehemu ya huduma kwa jamii, katika Shule
ya Msingi Ushindi iliyopo Mikocheni ‘B’, jijini Dar es Salaam jana.
Wanaoshuhudia (kutoka kushoto) ni Mwenyekiti wa Shule hiyo, Jumanne
Konara, Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Elias Katunzi, Mtendaji wa
Serikali ya Mtaa wa Mikocheni ‘B’, Suleiman Sagong’o na baadhi ya
wafanyakazi wa Airtel.
Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso (kulia),
akiwasalimia watoto baada ya kukabidhi Darasa la Chekechea
lililokarabatiwa kwa udhamini wa Wafanyakazi wa Airtel, kama sehemu ya
huduma kwa jamii, katika Shule ya Msingi Ushindi iliyopo Mikocheni
‘B’, jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Meneja wa Huduma kwa Jamii
wa Airtel, Hawa Bayumi.
Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso (kushoto), Meneja
wa Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (mwenye miwani), na Afisa
Mwandamizi wa Kitengo cha Biashara za Mashirika, Delfina Martin (mbele
kulia), wakiwa wamekaa na watoto baada ya kukabidhi Darasa la
Chekechea lililokarabatiwa kwa udhamini wa Wafanyakazi wa Airtel, kama
sehemu ya huduma kwa jamii, katika Shule ya Msingi Ushindi iliyopo
Mikocheni ‘B’, jijini Dar es Salaam jana.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Airtel Tanzania, wakigawa zawadi kwa
watoto baada ya kukabidhi Darasa la Chekechea lililokarabatiwa kwa
udhamini wa Wafanyakazi wa Airtel, kama sehemu ya huduma kwa jamii,
katika Shule ya Msingi Ushindi iliyopo Mikocheni ‘B’, jijini Dar es
Salaam jana.
Kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel kupitia mradi wake wa “Airtel
Tunakujali” wakishirikiana na wafanyakazi wa kitengo cha Airtel
Biashara za Mashirika wameendeleza dhamira ya kusaidia jamii
kwa kukarabati darasa la chekechea katika shule ya msingi Ushindi
iliyopo jijini Dar Es Salaam. Leo Airtel imebadili mtazamo wa darasa
hilo kwa kuwa jengo la kisasa na kuwapatia vitendea kazi ikiwemo
madawati na michezo mbalimbali kwa ajili ya watoto hao.
Shule ya Msingi Ushindi imekuwa miongoni mwa shule hapa nchini
zilizoweza kuingia katika mfuko wa mradi wa “Airtel Tunakujali” ili
kuboresha kiwango cha elimu hapa nchini. Baadhi ya shule ambazo
zilishaweza kuingia katika mradi huo ni Kumbukumbu Shule ya Msingi
iliyopo Kinondoni jijini Dar es salaam na shule ya Msingi Pongwe mjini
Tanga. Lengo la mpango huu ni kuboresha mazingira ya wanafunzi na
walimu mashuleni,kuwapataia wanafunzi elimu bora, kuhamasisha
mahudhurio mazuri ya wanafunzi mashuleni na kunyanyua kiwango cha
mfumo wa elimu katika katika taasisi hii.
Akizungumza katika hafla hiyo ya makabidhiano , Mkurugenzi mkuu wa
Airtel Tanzania Sunil Colaso alisema, "Kutokana na dhamira ya Airtel
tunafuraha kubwa sana kupata nafasi hii na kuwa ni wa moja wa
makampuni yaliyopata nafasi ya kujenga mazingira bora na imara katika
sekta ya elimu. Leo hii tunakabidhi darasa zuri na la kisasa lenye
Uwezo wa kukidhi idadi kubwa ya wanafunzi., hii itasaidia kupunguza
shida iliyopo na kufanya mazingira ya kusomea kwa wanafunzi wengi kuwa
rafiki. Tunaamini kwamba ubora wa elimu ni muhimu zaidi katika karne
hii kwa ajili ya maendeleo ya kijamii na kiuchumi hapa Tanzania. Sisi
pia tunatambua changamoto nyingi katika ngazi zote za sekta hii
muhimu.
Aliongeza " kwa kuboresha mazingira ya wanafunzi hawa ni kuchochea
uelewa na kuinua maisha yao ya hapo baadae. "Bila shaka, ubora wa
elimu unawapa watoto nafasi bora katika maisha kutambua ndoto zao na
kuwa viongozi bora wa kesho. Colaso aliendelea akisema, “anawaomba
walimu na wanafunzi wa Ushindi watunze rasilimali iliyotolewa kwao
ili viweze kutumika na watoto wengine watakaokuja hapo baadae”.
Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi ya Ushindi Elias Katunzi akitoa
shukrani zake kwa Airtel alisema ,”kwa niaba ya walimu, wazazi na
wanafunzi wa shule ya msingi ya Ushindi napenda kutoa shukrani zetu za
dhati kwa kuweza kututengenezea darasa lililobora na imara .
Ningependa kuwashukuru Airtel kwa yote waliyotufanyia kwa ajili ya
shule hii. Kutokana na msaada huu tuanaamini kabisa idadi ya watoto
itaongezeka kwani kwa sasa tunawatoto wapatao 50 wa
chekechea.Tunaamini kwamba idadi ya watoto itaongezeka na wazazi
watapata moyo zaidi wa kuwaandikisha watoto wao hapa shuleni.
Tunatarajia uandikishaji utaongezeka katika kipindi kitakachofwata
"alibainisha Katunzi.
Mwalimu mkuu akaongeza pia kuwa anafurahi kwamba Airtel wameweza
kuwasaidia katika tatizo hilo la ukarabati wa jengo na kuziomba
taasisi nyingine kuchangia sekta ya elimu katika shule mbalimbali
kwani matatizo yanafanana nchini kote.
0 comments:
Post a Comment