Na:George Binagi-GB Pazzo
Shule ya Msingi Green Hill iliyopo Ilala Mkoani Dar
es salaam imekuwa miongoni mwa shule bora zilizofanya vizuri katika mtihani wa
darasa la saba, uliofanyika mwezi Septemba mwaka huu kote nchini.
Katika Matokeo yaliyotangazwa jana na Katibu
Mtendaji wa Baraza la Mitihani nchini NECTA Dk.Charles Msonde, ufaulu wa Kitaifa
mwaka huu umepanda kwa asilimia 10.85 kutoka asilimia 56.99 za mwaka jana,
ambapo wanafunzi waliofaulu ni 518,034 kati ya 775,273 waliosahiliwa mwaka huu.
Kwa upande wa Matokeo ya Msingi Green Hill, Matokeo
yanaonyesha kuwa shule hiyo imeshika nafasi ya saba kati ya shule 56 katika
Wilaya ya Ilala, nafasi ya 39 kati ya shule 634 katika Mkoa wa Dar es Salaam na
nafasi ya 324 kati ya shule 16,096 Kitaifa.
Wahitimu wote 93 wa shule hiyo wakiwemo wa kume
ni 45 na wa kike 48 wamefaulu mtihani wao kwa madaraja yote ya ufaulu jambo
lililofanya shule hiyo kupokea pongezi mbalimbali kutoka kwa wazazi na walezi
wa wahitimu hao kwa njia mbalimbali ikiwemo mitandao ya kijamii.
0 comments:
Post a Comment