WANAFUNZI WA CHUO CHA UTUMISHI WA UMMA (TPSC) TAWI LATANGA WAFANYA ZIARA YA MAFUNZO PSPTB

1
Wageni wakiwasili kwenye ofisi za Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi.
New Picture (3)
Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa PSPTB, Dr Tesha akitoa hutuba ya ufunguzi kuwakaribisha wanachuo wa mwaka wa pili wa stashahada ya Ununuzi na Ugavi kutoka chuo cha TPSC Utumishi wa Umma tawi la Tanga.
New Picture (4)
Wanachuo wakimsiliza Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Bodi Dr. Tesha.
New Picture (5)
Mkurugenzi ya Mafunzo, Bw. Godfred Mbanyi akielezea juu ya madaraja ya mitihani ya Bodi na taratibu za kufanya mitihani.
New Picture (7)
Bw. Ally Songoro kutoka Kurugenzi ya Taaluma akifafanua jambo, juu ya taratibu za usajili, miiko ya wanataaluma kwa wanachuo waliotembelea Bodi.
New Picture (9)
Bw. Paul Bilabaye kutoka Kurugenzi ya Fedha na Utawala akielezea taratibu za malipo ya huduma mbalimbili zitolewazo na Bodi.
New Picture (10)
Mwanachuo mmoja akiuluza maswali juu ya kazi mbalimbali za Bodi Wataalam wa Ununuzi na Ugavi.
New Picture (11)
Mmoja wa wanachuo akiuliza maswali juu ya kazi mbalimbali za Bodi Wataalam wa Ununuzi na Ugavi.
New Picture (1)
Wanachuo wakiwa kwenye picha ya pamoja kwenye ofisi za Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi.
New Picture (2)
Baadhi ya wanafunzi kwenye picha ya pomoja pamoja na mkurugenzi Mkurugenzi mtendaji wa Bodi Dr. Clemence Tesha na viongozi waandamizi wa Bodi.
---
Na Mwandishi wetu

Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) imepokea ugeni wa wanachuo sabini wa mwaka wa pili wanaosoma stashahada ya ununuzi na ugavi waliokuja kwenye ziara ya mafunzo kutoka Chuo cha Utumishi wa Umma tawi la Tanga. 

Ziara hiyo ya mafunzo ililenga kujua kazi mbalimbali za Bodi ya wataalam wa ununuzi na Ugavi (PSPTB). Mkurugenzi mkuu Mtendaji wa PSPTB Dr Clemence Tesha, aliupokea ugeni huo, na kuwashukuru kwa kuona nia ya kufanya ziara ya mafunzo. 

Aidha aliwaelezea umuhimu wa kuzingatia maadili , kujifunza kwa bidii ili kupata maarifa na ujuzi unaoweza kuhimili soko la ushindani la ajira . Wanachuo pia walielezewa juu ya taratibu za mitihani ya Bodi yenye ngazi ya cheti cha awaliAwali, msingi Msingi na Taaluma. 

Aliwaelezea taratibu za kusajii kwa ajili ya kufanya mitihani ya kitaaluma mara baada ya kumaliza masomo yao na kwamba mhitimu wa stashahada ya ununuzi na ugavi kwa chuo kinachotambuliwa na Bodi anaanzia ngazi ya kwanza ya mitihani ya taaluma. 

Mitihani ya taaluma ina ngazi tano, ambazo huhitimishwa kwa wanafunzi kufanya mitihaniutafiti. Ziara hiyo pia ilitoa fursa kwa wanachuo hao kujua taratibu za kujisajili kama wataalum wataalam wa Ununuzi na Ugavi kwani ni hitaji la sheria iliyounda Bodi. Aidha walifahamishawa kwamba kuna ngazi mbalimbali za usajili ambazo zinatambua kiwango cha ujuzi na uzoefu wa mtaalam. “ fanyeni usajili mara mmalizapo chuo ili kutumia fursa za ajira katika fani yenu “ ” alisisitiza.  

Tambueni kwamba taaluma ya ununuzi na ugavi inaongozwa na misingi ya maadili ambayo inawataka kutambua kuwa mnawajibika kwa umma wa watanzania, taaluama yenu, mwajili wako. Misingi hii ya wajibu ndio inayoifanya taaluma hii iwe ya kipekee. “maadili huanzia
SHARE
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment