JE ULIPOSOMA SHULE YA MSINGI UNAPAKUMBUKA?? NA KURUDI KUJUA MAENDELEO...

 Anthony Peter Mavunde ni kijana mtanzania aliyezaliwa mkoani Dodoma na kupata elimu yake katika shule ya msingi Mazengo, pia amefanikiwa kusoma hadi kuwa mwanasheria na wakili wa kujitegemea.

Wakili Anthony Mavunde jana alitembelea shule yake ya Msingi aliposoma ikiwa ni katika kutaka kujua changamoto zinazoikabili shule yake hiyo... haya ndiyo maneno ya kijana huyu machachari mwenye malengo ya kuwa kiongozi katika Taifa letu siku za mbeleni. 

  "Leo asubuhi nimetembelea Shule ya Msingi Mazengo, shule niliyosoma darasa la I-VII kwa lengo la kubaini changomoto mbalimbali zinazoikabili shule. Nimekubali kuchukua jukumu la kuwatafuta wenzangu wote waliopitia shule ya Msingi Mazengo kwa lengo la kusaidia kutatua changamoto mbalimbali.
Hatua ya kwanza, Tunakusudia kukarabati vyoo na kupaka rangi majengo ya shule na pia kuboresho kitengo cha IT. Kwa kuanzia nimeahidi kuchangia Laptop moja na namshukuru kaka yangu Tumaini Mtei kwa kukubali kuchangia printer. Niwaombe wana Mazengo wote tujitokeze kusaidia. "Mwisho wa kumnukuu wakili huyo.
SHARE
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment