Kaimu Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Changamoto za Milenia (Millenium Challenge Account - MCAT) Eng. Salum Sasilo (kulia) akimkabidhi funguo Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya - MUST Prof. Joseph Msambichaka kama ishara ya makabidhiano rasmi ya kambi ya Kianda iliyokuwa ikitumiwa na Mkandarasi Aasleaf Bam International katika ujenzi wa barabara ya lami kuunganisha Mikoa ya Rukwa na Mbeya katika mradi wa Laela - Sumbawanga wenye jumla ya Kilomita 95. Chuo hicho Kikuu cha MUST kimedhamiria kubadilisha kambi hiyo yenye jumla ya ekari 118 na majengo ya kudumu zaidi ya 18 kuwa moja ya Kampasi zake itakayobobea katika sekta ya uhandisi ujenzi hususani ujenzi wa barabara.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya akitoa salamu zake katika hafla hiyo ambapo ameitaka taasisi ya MUST kuhakikisha kuwa inatunza miundombinu waliyokabidhiwa na kuiendeleza kwa ajili ya kusaidia sekta ya elimu nchini kwa vizazi vilivyopo na vijavyo. Aliongeza kuwa dhamira ya Serikale yake ya Mkoa ilikua ni kuona kambi hiyo inakabidhiwa kwa moja ya taasisi kubwa za elimu nchini ikiwemo Chuo Kikuu cha Dar es Salaamn na taasisi zingine ili kuinua sekta ya elimu nchini lakini imekuwa bahati kwa chuo cha MUST kupata nafasi hiyo ambayo ni muhimu kwa maendeleo ya chuo chao na elimu kwa ujumla. Amekiomba Chuo hicho kuona uwezekano wa kuipa Kampasi hiyo ya Kianda jina la Rukwa kwa ajili heshma ya maeneo hayo ambayo yapo Mkoani Rukwa katika Wilaya ya Sumbawanga.
Meza kuu.
Picha ya pamoja.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya katikati akizungumza na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya - MUST Prof. Joseph Msambichaka kulia na Meneja Mradi wa Kampuni ya Aasleaf Bam International iliyojenga barabara ya Lami ya Laela - Sumbawanga Ndugu Russel Rourke muda mfupi baada ya zoezi la makabidhiano ya kambi hiyo ya Kianda.
(Na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa@Rukwareview.blogspot.com)
0 comments:
Post a Comment