Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi Kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Richard Kayombo akitoa neno kuwakaribisha wageni katika mkutano wa Kwanza wa Wakuu wa Vyuo vya Kodi Afrika uliohudhuriwa na wajumbe zaidi ya 50 kutoka katika taasisi za kodi barani Afrika, Mkutano huo umeandaliwa kwa ushirikiano wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Taasisi za Kodi Afrika (ATAF), leo Jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Kodi Tanzani (ITA) Prof. Isaiah Jairo akiongea na wajumbe wa mkutano huo na kueleza namna utakavyosaidia katika kuzijengea uwezo Taasisi za ukusanyaji kodi Afrika hivyo kuweza kuinua uchumi wa Mataifa mengi ya Afrika.
Mkurugenzi wa Ujengaji Uwezo kutoka Taasisi za Kodi Afrika (ATAF) Bw. Kennedy Onyonyi akiwaeleza wajumbe wa Mkutano huo namna Kamati hiyo inavyoshirikiana na Taasisi za Kodi Afrika katika kuzijengea Taasisi hizo uwezo wa Kiutendaji na kusaidia nchi wanachama kushiriki kuwa na sera ya pamoja ya masuala ya Kodi ili kuongeza ufanisi katika ukusanyaji kodi.
Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Lusekelo Mwaseba Akiongea na wajumbe waliohudhuria Mkutano huo namna Tanzania ilivyofurahishwa na kuwa mwenyeji wa Mkutano huo wa Kwanza wa wakuu wa vyuo vya uongozi wa Kodi Afrika na kuwataka wajumbe kutumia fursa hiyo kujifunza masuala mbalimbali katika sekta hiyo ya ukusanyaji kodi kwani ni moja ya mhimili muhimu wa maendeleo kwa Mataifa mengi duniani.
Wakuu wa vyuo vya uongozi wa Kodi Barani Afrika wakiwa katika picha ya pamoja
Mkurugenzi Ujengeaji Uwezo kutoka Taasisi za Kodi Afrika (ATAF) Bw. Kennedy Onyonyi akiwasilisha Mada wakati wa Mkutano huo wa kwanza unaofanyika Nchini Tanzania.
PICHA NA HASSAN SILAYO - MAELEZO.
0 comments:
Post a Comment