MBUNGE WA JIMBO LA TEMEKE ABBAS MTEMVU ATOWA MADAWATI 270 KWA SEKONDARI ZA JIMBO LAKE

 Mbunge wa Jimbo la  Temeke, Abbas Mtemvu akikabidhi madawati na  Mkuu wa Chuo cha Mafunzo na Ufundi Stadi (Veta) , Samuel Ng'andu, Dar es Salaam jana, baada ya mbunge huyo kuamua kununua madawati 270 kwa ajili ya shule za sekondari zilizopo Jimboni kwake akiongozana na Madiwani wa Jimbo hilo.
 Baadhi ya madawati 270 yaliyonunuliwa na Mbunge wa Jimbo la Temeke kwa Shule za Sekondari zilizopo Jimboni kwake ambapo madawati 100 yalikwisha chukuliwa kupelekea jumla ya madawati 300 yenye jumla ya Sh. Mil 60 (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA)
 Mbunge Abbas Mtemvu akiongea na Waandishi wa Habari (pichani hawapo) baada ya kununua madawati katika Chuo cha Ufundi Stadi (Veta) na kuwakabidhi Madiwani  wa Jimboni kwake
Diwani Kata ya Keko Frances Mtawa (kushoto) ,  akimshukuru Mkuu wa chuo hicho cha Veta kuwa mwepesi kuwasikiliza  na akatumia nafasi ya kumshukuru Mbunge wake Abbas Mtemvu kwakuwa muwazi na kuwashirikisha madiwani wa jimbo hilo, kulia ni Mkuu wa chuo cha Ufundi Stadi Veta na katikati ni Mbunge wa Jimbo la Temeke Abbas Mtemvu
SHARE
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment