Mmoja wa Wanafunzi wa Shule ya Msingi Kiseke - Elias Sita anaye soma darasa la Nne, akifurahi
pamoja na Afisa Mkuu wa Fedha wa NMB - Bw. Waziri Barnabas baada ya shughuli ya makabidhiano
ya madawati shuleni hapo.
Bw. Daniel Makorere, Afisa Elimu Wilaya ya Ilemela Mkoani Mwanza akimshukuru Afisa Mkuu wa
Fedha wa NMB Bw. Waziri Barnabas(kushoto) baada ya kupokea madawati yenye thamani ya shilingi
milioni 5 kutoka benki ya NMB. Msaada huo wa madawati ulikabidhiwa kutoka NMB kwa Shule ya
Msingi Kiseke ili kupunguza uhaba wa madawati unaoikumba shule hiyo. Wakishuhudia kutoka kulia
ni Meneja wa NMB Kanda ya Ziwa Bw. Abraham Augustino pamoja na Mwalimu Mkuu wa Shule ya
Msingi Kiseke Bw, Denitrus Wima.
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Kiseke Wilaya ya Ilemela Mkoani Mwanza, wakiwa wameketi
kwenye madawati 64 yenye thamani ya shilingi milioni 5 waliyokabidhiwa na Benki ya NMB kama
sehemu ya msaada kwa shule hiyo.
0 comments:
Post a Comment