UKOSEFU WA CHAKULA MASHULENI WACHANGIA UTORO

 
Na Woinde Shizza, Arusha.

Ukosefu wa Chakula sheleni hususan zile zinazomilikiwa na serikali umetajwa kuwa chanzo kikubwa kinasababisha wanafunzi kutoroka
mashuleni na kwenda kujitafutia chakula hali inayoathiri taaluma na
maendeleo ya elimu nchini.


Mwanakijiji wa kijiji cha Arkata  Kipara Ngine amesema kuwa watoto
wengi wamekua wakitoroka shuleni kwa kukosa chakula hivyo kupelekea
idadi ndogo ya mahudhurio  mashuleni.

Kipara ameihasa saerikali kwa kushirikiana na mashirika binafsi pamoja na wazazi kuhakikisha upatikanaji wa chakula  katika sahule ya msingi
Arkata iliyopo wilaya ya Monduli mkoani hapa.

Mwenyekiti wa Kamati ya  Shule Kipi Alarosi  amesema kuwa licha ya changamoto ya utoro bado shule hiyo inakabiliwa na uchakavu wa majengo na upungufu wa madarasa hivyo ameiomba jamii na wapenda maendeleo wajitokeze kuiwezesha shule hiyo iweze kufanya vizuri kitaaluma.

“Shule haina madirisha na majengo yamechakaa mvua ikinyesha inaingia mpaka darasani watoto hawasomi vizuri hata kipindi cha jua vumbi
linajaa darasani “ Alisema Mwenyekiti.

Mkurugenzi wa Shirika la wafugaji Monduli Pastoralist Development (MPDI) Erasto Sanare  amesema kuwa baada ya kupokea ombi la shule hiyo
watatua fedha za ukarabati wa  madarasa ya shule hiyo ili kuwajengea
watoto mazingira bora.

Alisema mwamko wa jamii ya wafugaji katika masomo umekua kwa kiasi kikubwa  mashirika na watu binafsi yakijitoa kusaidia kutatua
changamoto zao ili watoto wa wafugaji wapate elimu bora.
SHARE
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment