Modesta Joseph, mwananfunzi wa
Kisutu Sekondari Dar es Salaam akipeana mkono wa pongezi na hati ya fedhana
John Mngodo, Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia
baada ya kushinda tuzo ya ubunifu wa TEHAMA wa kuwawezesha wananfunzi
kuwasilisha kero zao za usafiri kutumia TEHAMA kwa Taasisi ya EWURA.
Mgimba Faustine akipokea tuzo ya
fedha taslimu kutoka kwa Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na
Teknolojia baada ya kushinda Tuzo ya Wabunifu wa TEHAMA ya kuwawezesha wateja
kutumia simu ya mkononi kubaini bidhaa feki. Anayeshuhudia katikati ni Naibu
Balozi wa Finland nchini Tanzania Mhe. Simo-Pekka Parviainen na wa pili kulia
ni Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia Dkt. Hassan
Mshinda
Kaimu Katibu Mkuu wa
Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia akimpatia Japhet Sekenya tuzo
ya wabunifu wa TEHAMA kwa kutengeneza mtindi kwa kutumia karanga na
unaoweza kutibu magonjwa mbali mbali ya binadamu kama vile vidonda
tumboni, kuzuia saratani. Wa tatu kulia Naibu Balozi wa Finland nchini
Tanzania Mhe. Simo-Pekka Parviainen akishuhudia tukio hilo pamoja na
Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH (Wa pili kulia), Dkt. Hassan Mshinda.
0 comments:
Post a Comment