Mkurugenzi mtendaji wa Global Education Link akiwapa maelezo wananchi alipotembelea banda la Global Education Link katika maoneho ya wiki ya elimu ya vyuo vikuu katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Da es Salaam.
Wanafunzi wakipata maelekezo walipotembelea maoneho ya wiki ya elimu ya vyuo vikuu katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Da es Salaam.
Na Mwandishi Wetu
Kaimu mkurugenzi mtendaji wa shirika la taifa la bima (NIC), Sam Kamanga akipata maelezo kutoka kwa afisa masoko mwandamizi wa shirika
la taifa la bima (NIC),Joyce Mswia katika maoneho ya wiki ya elimu ya
vyuo vikuu katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Da es Salaam.
---Na Mwandishi Wetu
Watanzania wametakiwa kuangalia ubora elimu katika vyuo vya nje na sio kuangalia majina ya vyuo hivyo ili ukuweza kupata wataalamu wataosaidia nchi kupata maendeleo.
Hayo aliyasema jana, Mkurugenzi Mtendaji wa Global Education Link, Abdulmaliki Mollel katika maonesho ya Elimu ya Vyuo Vikuu vya Ndani na Nnje ya nchi yanayofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam.
Mollel amesema yeye akiwa wakala wa vyuo vikuu vya nje anatambua vyuo walivyoenda watanzania kusoma hawakumuangusha kutokana na kujituma kwao pamoja na mazingira rafiki ya kusomea katika vyuo hivyo.
Amesema watu wanaokwenda katika vyuo kwa kuangalia majina wanarudi na kuwa hawana msaada wa elimu walioipata nje na kulazimika nchi kuchukua wataalam kutoka nje wenye uwezo kutokana na vyuo vyao na kuacha watanzania waliopata elimu katika vyuo vyenye majina lakini havina elimu bora.
Mollel amesema kuna vyuo vingi nje lakini suala la kuangalia ubora wa elimu inayotolewa na mazingira ya kusomea kutokana na baadhi ya watu waliosoma wamekuwa wakiiga utamaduni mwingine na kuingiza nchini na kushindwa kuendana na utamaduni wa ndani na kusababisha kukosa ajira.
Mollel amewataka watanzania kutumia Global Education Link katika kuweza kuwapa vyuo bora ambavyo itasaidia vijana kupata elimu bora kutokana na uwezo wa vyuo husika.
Aidha amesema Global Education Link imekwenda mbali zaidi kwa baadhi ya vyuo vya nje kuingiza kozi katika vyuo vya ndani ikiwemo kozi ya Petrol, Gesi.
Amesema anafanya kazi na vyuo 10 vya nje ambavyo vinazalisha elimu bora yenye kumsaidia mtanzania katika kuweza kuongeza uwezo wa kitaalam katika nchi.
0 comments:
Post a Comment