Mkurugenzi Msaidizi Lugha, Idara ya Maendeleo ya Utamaduni kutoka Wizara ya
Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Hajjat Shani Kitogo aliyenyoosha mikono akiongea na
baadhi ya wanafunzi wa darasa la saba wa shule ya msingi Mtendeni iliyopo jijini Dar es
Salaam wakati timu ya Wizara ilipotembelea shule hiyo kufanya utafiti kuhusu Majina
Fiche.Majina Fiche ni majina yanayotolewa kwa njia ya mafumbo baada ya kutokea kisa au
mkasa Fulani kwa jamii ikiwa na lengo la kukuza na kuendeleza lugha ya Kiswahili na lugha za
jamii.
Afisa Utamaduni Mila na Desturi Idara ya Maendeleo ya Utamaduni kutoka Wizara ya
Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Elizabeth Hizza aliyesimama kulia akiongea na
baadhi ya wanafunzi wa darasa la saba wa shule ya msingi Mtendeni iliyopo jijini Dar es
Salaam juu ya umuhimu wa mila na Desturi nzuri za Mtanzania.
Afisa Utamaduni Lugha Idara ya Maendeleo ya Utamaduni kutoka Wizara ya Habari,
Vijana, Utamaduni na Michezo Bw. Christopher Mhongole akiongea na baadhi ya wanafunzi
wa darasa la saba wa shule ya msingi Mtendeni iliyopo jijini Dar es Salaam juu ya umuhimu wa
kuwa na Majina Fiche katika jamii ikiwa ni juhudi za kukuza mila na desturi za Mtanzania.
Afisa Utamaduni Mila na Desturi Idara ya Maendeleo ya Utamaduni kutoka Wizara ya
Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bw. Boniface Kadili akiongea na baadhi ya wanafunzi
wa darasa la saba wa shule ya msingi Mtendeni iliyopo jijini Dar es Salaam juu ya umuhimu wa
mila na Desturi nzuri za Mtanzania.
0 comments:
Post a Comment