WANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI MUHIMBILI 1988 WAIKUMBUKA SHULE YAO

Mgeni Rasmi Balozi Kassimu Mwawado, akikata utepe ili kufungua Ofisi ya walimu wa shule ya msingi Muhimbili, iliyokarabatiwa na kuweka viti 29 na meza 8 na wanafuzi waliohitimu darasa la saba katika shule hiyo Mwaka 1988, pamoja na kiti na meza ya kisasa katika ofisi ya Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo katika hafla fupi iliyoandaliwa na wanafunzi hao ikiwa imeudhuliwa na walimu wa shule hiyo wa tangu mwaka 1978.
 Walimu wa Shule ya Msingi Muhimbili wakifurahia kupewa viti vipya pamoja na meza na wanafunzi wao waliohitimu shule ya msingi mwaka 1988 katika shule hiyo, wamekabidhiwa Samani hizo leo katika shule hiyo jijini Dar es Salaam.
 Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Muhimbili, Dafrosa Assenga akipeana mkono na Mgeni Rasmi Balozi Kassimu Mwawado, mara baada ya kukabidhiwa kiti na meza Mpya kutoka kwa wanafunzi walihitimu katika shule hiyo Mwaka 1988, ikiwa ni mchango wao katika kuendeleza elimu katika shule hiyo. Kutoka kulia ni Muhitimu wa shule ya msingi Muhimbili mwaka 1988 na Mkurugenzi wa Galaxy Cargo, Jonatha Kasesele, Mwenyekiti wa wahitimu 1988  shule ya msingi muhimbili,Usia Mkoma
Mwalimu mstaafu katika shule ya msingi Muhimbili wa mwaka 1972-2012, Amani Ndussy na  Mwenyekiti wa bodi shule ya msingi Muhimbili, George Ntevi.
Mwalimu mstaafu katika shule ya msingi Muhimbili wa mwaka 1972 - 2012, Amani Ndussy akizungumza mara baada ya wanafunzi wa hitimu wa sarasa la saba mwaka 1988 katika shule hiyo kukabidhi viti vya walimu pamoja na meza, katika hafla fupi iliyoandaliwa na wanafunzi hao katika shule hiyo jijini Dar es Salaam leo. 
Mwalimu wa shule ya msingi Muhimbili wa mwaka 1986 hadi sasa, Marry Massawe akiwashukuru wanafunzi waliosoma shule hiyo kwa kuikumbuka shule yao.
Wanafunzi wa shule ya msingi Muhummbili mwaka huu wakiwa wamehudhulia hafla fupi ya wahitimu wa shule hiyo mwaka 1988 leo jijini Dar es Salaam.
 Wanafunzi wa shule ya msingi Muhimbili wakiimba wimbo kuwashukuru wanafunzi wa zamani katika shule hiyo kwa kuwakumbuka waalimu wao pamoja na shule yao.
Baadhi ya wanafunzi waliomaliza katika shule ya Msingi Muhimbili wakiwa wamehudhuria hafla fupi pamoja na waalimu wao, katika shule hiyo jijini Dar es Salaam leo.
SHARE
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment